IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu India

Watu wa Bangladesh wataka nchi za Kiislamu kukata uhusiano na India

12:47 - June 11, 2022
Habari ID: 3475363
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya watu waliandamana katika mji mkuu wa Bangladesh wa Dhaka siku ya Ijumaa kulaani matamshi ya hivi majuzi ya matusi ya maafisa wa chama tawala India kuhusu Mtukufu Mtume Muhammad SAW.

Waandamanaji waliokuwa na hasira walihimiza mataifa yenye Waislamu wengi kukata uhusiano wa kidiplomasia na India na kususia hadi pale itakapochukua hatua kali  kuwwadhibu maafisa wawili wa chama tawala kwa matamshi hayo ya matusi.

Waandamanaji pia waliikosoa serikali ya Bangladesh kwa kutokosoa hadharani matamshi hayo ya maafisa wa India dhidi ya Mtume Muhammad SAW.

Waliandamana baada ya sala ya Ijumaa kupitia mitaa karibu na Msikiti mkuu wa Baitul Mukarram katikati mwa jiji la Dhaka. Wengi walisikika wakitoa kauli mbiu dhidi ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi huku hasira ikiongezeka nchini Bangladesh na mataifa mengine yenye Waislamu wengi tangu wiki iliyopita, wakati maafisa wawili wa Chama tawala cha Bharatiya Janata (BJP) chenye misimamo mikali ya Kihindu walipotoa maoni hayo ya matusi.

Chama cha Modi kimemsimamisha kazi afisa mmoja na kumfukuza mwingine, huku kikisema kinalaani matusi ya watu watukufu katika dini, lakini waandamanaji wa Bangladesh walisema hatua hizo hazitoshi.

Walimsihi Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina kutoa tamko rasmi la kulaani serikali ya Modi katika Bunge, ambalo linafanya kikao chake cha bajeti.

Hasina amedumisha uhusiano mzuri na India kwa zaidi ya muongo mmoja licha ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya India huko Bangladesh, taifa lenye Waislamu wengi lenye watu milioni 160. India ni jirani wa Bangladesh na mshirika mkuu wa biashara.

3479246

Kishikizo: bangladesh hasina bjp india
captcha