IQNA

Utamaduni wa Qur'ani

Wairani wanategemea mafundisho ya  Qur'ani katika kupambana na madola ya kibeberu

21:08 - December 17, 2024
Habari ID: 3479911
IQNA – Mbunge mmoja nchini Iran amesema kutekeleza mafundisho ya Sunnah za Qur'ani (sharia) kumewapa Wairani roho ya kusimama dhidi ya madola yenye kiburi na ya kibeberu.

Ruhollah Motefaker Azad ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwa washiriki katika hatua ya mwisho ya Mashindano ya Kitaifa ya Quran ya Iran ya 47 Jumapili jioni. 

Sehemu ya wanaume ya mashindano hayo inaendelea katika mji wa Tabriz ulioko kaskazini-magharibi. 

Kilichowezesha Wairani kuanzisha mapinduzi yaliyoongozwa na Imam Khomeini (RA) ili kueneza Uislamu na Tauhidi ni mafundisho ya Quran Takatifu, amesema Motefaker Azad. 

Aidha amesema kwamba maisha ya ubinadamu yana mafanikio tu  katika kujifunza Quran. 

Ameongeza kwamba kuandaa mashindano haya ya Qur'ani na matukio kama haya kunaonyesha kuwa kiini cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimechanganyika na mafundisho ya Qur'an Takatifu. 

Mwenyezi Mungu anatufundisha kupitia Qur'ani Tukufu na Ahl-ul-Bayt (AS) jinsi ya kuishi, alisisitiza zaidi katika hotuba yake. 

Mwakilishi huyo wa watu wa Tabriz, Azarshahr na Osku katika Majlisi ya Ushauri ya Kiisalmu, yaani Bunge la Iran, aliongeza kusema kuinua utamaduni wa Qur'ani kutawezesha kuishi maisha ya kiroho na yanayotegemea Qur'ani.

3491077

captcha