IQNA

Harakati za Qur'ani

Ufafanuzi kuhusu shughuli za Qur'ani za Taasisi ya Diyanet ya Uturuki

21:21 - May 21, 2023
Habari ID: 3477027
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa banda la Kurugenzi ya Masuala ya Kidini ya Uturuki (Diyanet) katika Maonyesho ya 34 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran amesema Diyanet inatekeleza shughuli mbalimbali za Qur'ani Tukufu duniani kote.

Akizungumza katika mahojiano na IQNA, alisema Diyanet ni taasisi yenye mfungamano na serikali ya Uturuki na ina jukumu la kuandaa na kusimamia masuala ya kidini nchini humo.

Kusimamia shughuli za misikiti na vituo vya kidini, kutoa mafunzo kwa wasomi wa kidini na maimamu wa misikiti, na kutoa vyeti kwa wahifadhi Qur'ani na Hadith, ni kati ya majukumu ya taasisi hiyo alisema.

Miongoni mwa shughuli kuu za taasisi hii pia uchapishaji wa vitabu vya kidini, ambavyo hufanywa katika kitengo maalumu cha uchapishaji cha taasisi hiyo, alibaini.

Aliongeza kuwa Diyanet pia inaendesha maduka makubwa 40 ya vitabu ambayo yanasambaza vitabu vya kidini vilivyochapishwa kwa Kituruki.

Kuchapisha na kusambaza nakala za Quran pamoja na tafsiri ya Kitabu hicho kitukufu ni miongoni mwa shughuli za Diyanet, alisema.

Shirika hilo pia linaendesha shughuli za kutoa misaada kama vile kuchapisha Qur'ani Tukufu na tafsiri yake katika lugha tofauti kwa wale wanaozihitaji katika mataifa mengine, afisa huyo alibainisha.

Amesema aghalabu ya Misahafu hiyo imesambazwa miongoni mwa Waislamu katika nchi za Kiafrika.

Hadi sasa, imetoa takriban nakala milioni tano za Qur'ani Tukufu na tafsiri zake kwa Waislamu wa Afrika, alisema.

Diyanet inalenga kutafsiri Qur'ani Tukufu katika lugha 70 na hadi sasa tafsiri za Kitabu hicho Kitakatifu katika lugha 27 zimekamilika, kulingana na afisa huyo.

Kwingineko katika mahojiano hayo, alipoulizwa kuhusu maonyesho hayo ya vitabu mjini Tehran, alipongeza mahudhurio mazuri ya maonyesho hayo na wananchi wa Iran.

Duru ya 34 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran ilifanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Musalla Imam Khomeinikuanzia tarehe 10 hadi 20 Mei.

4142058

captcha