IQNA

Jinai

Al Azhar yalaani hujuma ya kigaidi Ujerumani, utambulisho wa gaidi wabainika

23:14 - December 21, 2024
Habari ID: 3479933
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimelaani shambulio la kigaidi lililoua watu wawili na kujeruhi makumi kadhaa huko Magdeburg nchini Ujerumani.

Kuwashambulia raia na kuwatia hofu, bila ya kujali dini au imani zao, ni jinai mbaya inayoakisi kujitenga na mafundisho ya dini na tunu za kibinadamu na kimaadili zinazosisitiza uhifadhi wa maisha ya binadamu na uanzishwaji wa madaraja ya kuishi pamoja baina ya watu. Azhar alisema katika taarifa siku ya Jumamosi..

Gari moja lilipita katika soko la Krismasi katikati mwa mji wa Magdeburg nchini Ujerumani siku ya Ijumaa jioni na kuua watu 11 na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Wakati huo huo, Polisi ya Ujerumani imetangaza kuwa shambulizi soko la Krismasi huko Magdeburg halina mfungamano au msukumo wowote wa 'Kiislamu'.

Kwa mujibu wa tovuti ya T-Online, watu 11 waliuawa na wengine 60 kujeruhiwa katika hujuma hiyo.

Televisheni ya NTV imenukuu kauli ya mamlaka katika jimbo la shirikisho la Saxony-Anhalt kwamba "Dereva wa gari hilo aligonga umati wa watu kwenye soko la Krismasi huko Magdeburg, na kwamba ametiwa nguvuni.

Gaidi mzaliwa wa Saudi Arabia aliyehusika na shambulio la soko la Krismasi huko Magdeburg ametambuliwa kama Talib Al-Abdulmohsen.

 Talib ni Muislamu wa zamani anayeishi Ujerumani, na ni maarufu kwa machapisho yake ya mara kwa mara ya kupinga Uislamu na kutetea Uzayuni kwenye mitandao ya kijamii.

Jarida la Ujerumani Der Spiegel limeripoti kwamba mhalifu huyo ni daktari aliyebobea katika tiba ya kisaikolojia na anaunga mkono fikra za chama cha mrengo wa kulia cha Alternative for Germany.

Talib anatafutwa na Saudi Arabia kwa tuhuma zinazohusiana na ugaidi na biashara ya binadamu inayohusisha watu binafsi kutoka Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba ya Uajemi kelekea kwenye nchi za Umoja wa Ulaya (EU).

 Ujerumani ilikataa kumrejesha Saudi Arabia na badala yake ikampa hifadhi ya kisiasa mwaka 2006.

3491135

captcha