IQNA

Qur'ani Tukufu nchini Misri

Uzinduzi wa vikao vya Qur'ani vya Al-Azhar kwa walimu na waliohifadhi Qur’ani Misri

19:41 - August 22, 2022
Habari ID: 3475665
TEHRAN (IQNA)- Idara Kuu ya Masuala ya Qur'ani ya Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar ilitangaza kuanza kwa shughuli za vikao vya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya walimu na waliohifadhi Qur'ani wa vituo vyenye uhusiano na kituo hiki kote Misri.

Mpango huu umeanzishwa katika vituo tanzu vya Al-Azhar katika mikoa yote ya Misri, na madhumuni yake ni kuimarisha ujuzi wa walimu wa Qur'ani katika kusoma Qur'ani Tukufu.

Katika mpango huu, walimu mashuhuri na waliobobea wa Qur'ani wana jukumu la kufundisha stadi za usomaji na tajwid kwa washiriki, na pia wanawafundisha wanafunzi jinsi ya kuweka mazingira ya kufaa kwa ufundishaji sahihi wa aya za Qur'ani.

Mradi huu umetekelezwa chini ya usimamizi wa Sheikh Ahmed Al-Tayeb, Sheikh Mkuu wa Al-Azhar huku Mohammad Al-Dawaini, Makamu wa Rais wa Al-Azhar na pia Salama Dawood, Mkuu wa Idara ya Vituo vilivyounganishwa na Al-Azhar, pia walifuatilia kwa karibu mradi huu.

Ikumbukwe kuwa kabla ya hapo Wizara ya Wakfu ya Misri ilitangaza kufanyika mikutano ya usomaji wa Qur'ani kwa kushirikisha wanachuoni na wasomaji wakubwa wa nchi hii katika misikiti ya Cairo, na wizara hii pia iliandaa majlisi nne maalum za Qur'ani kwa wanawake

Mwaka huu, Wizara ya Wakfu ya Misri imetekeleza programu nyingi za kuongeza shughuli za Qur'ani nchini humo, miongoni mwa shughuli muhimu zaidi ni pamoja na kuunda duru maalum za Qur'ani za majira ya kiangazi, duru za Qur'ani za watoto na wiki mbalimbali za kitamaduni kwa kuwepo wasomaji mashuhuri  na hotuba za wanachuoni na watafiti katika uwanja huo.

4079961

Kishikizo: qurani tukufu al azhar
captcha