Kuna mjadala au maswali kuhusu ni kwa nani Waislamu wanapaswa kurejea baada ya kufariki Mtume Muhammad (SAW).
Utekelezaji kamili wa malengo ya Kiislamu hauwezekani bila ya kuwepo kwa mpangilio mpana wa kijamii kwa sababu Uislamu ni dini inayozingatia masuala yote ya maisha ya kibinafsi na ya kijamii ya watu na inaongoza mambo yao yote kwa kufuata Tauhudu na na kumwabudu Mwenyezi Mungu.
Kwa kuwa mitazamo na Hadith tofauti haziwezi haziwezi kukidhi kikamilifu hitajio hilo , Qur’ani Tukufu inawaagiza Waislamu ifuatavyo: “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. “. (Aya ya 103 ya Surah Al Imran)
Katika aya mbili zilizotangulia (101 na 102 za Al Imran), Qur’ani Tukufu inatanguliza kukimbilia kwa Mtukufu Mtume (SAW) na Aya za Mwenyezi Mungu kama dhamana ya mwongozo.
“Na vipi mkufuru hali nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu na Mtume yuko kati yenu? Na mwenye kushikamana na Mwenyezi Mungu basi huyo ameongozwa kwenye Njia Iliyo Nyooka. Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife ila nanyi ni Waislamu.”
Katika Surah An-Nisa vile vile, Qur’ani Tukufu inasisitiza kumfuata Mtume (SAW) katika mambo yote ya jamii na kinasema kukubali hukumu yake ni sharti la imani ya kweli: “La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.” (Aya ya 65 ya Surat An-Nisaa)
Lakini ni upi mfano wa "Kamba ya Mwenyezi Mungu" na nguzo ya utaratibu wa jamii baada ya Mtukufu Mtume (SAW)?
Qur’ani Tukufu inatanguliza dhana ya Ulul Amr na inatuamuru kuirejelea pale panapotokea tofauti na migongano na katika kuelewa na kuchambua masuala tata:
“Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu.” (Aya ya 83 ya Surat An-Nisaa)
Walii Amr, kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, ni wale ambao hawajapata wahyi lakini lazima wafuatwe na watu kama vile Mtukufu Mtume (SAW) alivyofuatwa: “Enyi mlio amini, mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka miongoni mwenu.” (Aya ya 59 ya Surah An-Nisa) Katika Aya inayofuata, imesisitizwa kwamba Ulul Amr hawatoi hukumu ambayo ni tofauti na ile iliyotolewa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (SAW).
Hakuna sharti la kumtii Ulul Amr na ukweli kwamba kuwatii ni sawa na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (SAW) kunaonyesha kuwa wao ni maasum katika kauli na vitendo. Kwa sababu hatuna uwezo wa kuzipambanua, tunapaswa kurejea kwa Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume (SAW) ili kuzijua na kuna Hadithi nyingi katika suala hili.
Mojawapo ni Hadiyth ya Thaqlayn, ambayo kwa mujibu wake, Mtume Mtukufu wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema: “Ninawaachia vitu viwili vya thamani (Thaqalayn), maadamu nyinyi mtashikamana navyo hamtapotea kamwebaada yangu. Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Itrah yangu, Ahl-ul-Bayt wangu. Havitatengana mpaka vinifika katika Hodhi (ya Kawthar peponi), basi angalia jinsi utakavyoamiliana navyo baada yangu.”
3488256