IQNA

Wasio Waislamu Wanaweza Pia Kunufaika na Mafundisho ya Eid Al- Ghadir

19:13 - June 24, 2024
Habari ID: 3479011
IQNA - Katibu Mkuu wa Majlisi ya Ulimwengu ya Ahl-ul-Bayt (AS) amesema si Waislamu pekee bali hata wasio Waislamu wanaweza kufaidika na mafundisho ya Tukio la Ghadir.

Ayatullah Reza Ramezani aliyasema hayo katika mkutano wa shakhsia wakuu wa kidini na vyombo vya habari pamoja naye mjini Qom siku ya Jumamosi. 

Kwa kuwa; fundisho la kwanza la Eid Ghadir ni kwamba watu bora na wanaofaa zaidi wawekwe katika nafasi za uwajibikaji kama ilivyokuwa siku ya Eid al-Ghadir wakati mbora wa watu alipoteuliwa kuwa kiongozi wa Ummah baada ya Mtume Mtukufu (saw).

Kwa mujibu wa Khatibu huyo, fundisho jingine la Eid  Ghadir ni kwamba watu wanapaswa kushiriki katika kutengeneza hatima yao wenyewe, na kuongeza kuwa suala la demokrasia ya kidini chimbuko lake ni mafundisho ya Ahl-ul-Bayt (AS).

Mkutano huo ulikuja kabla ya Eid al-Ghadir, ambayo itaadhimishwa siku ya Jumanne, mwezi  Juni 25, mwaka huu.

Tukio la Eid al-Ghadir huadhimishwa na Waislamu wa Shia duniani kote kila mwaka.

Ni miongoni mwa sikukuu muhimu na likizo za furaha za Waislamu wa Shia zilizofanyika siku ya 18 ya Dhul Hijjah katika kalenda ya mwandamo ya Hijri.


Khatibu huyo,akisisitiza Kusherehekea Eid al-Ghadir Kukuza Mafundisho ya Ahl-ul-Bayt
Ilikuwa ni siku ambayo kwa mujibu wa ripoti Mtume Mtumue (SAW) alimteua Ali Ibn Abi Talib (AS) kama khalifa wake na Imam baada yake mwenyewe kwa kufuata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kwingineko katika matamshi yake Ayatullah Ramezani ameashiria shughuli za Majlisi ya Ulimwengu ya Ahl-ul-Bayt (AS) na kusema inajitahidi kukuza na kufafanua mafundisho ya Ahl-ul-Bayt (AS) kimataifa.

Aliongeza kwa kusema kuwa; shughuli za mkutano huo zinajumuisha zaidi ya nchi 140 ulimwenguni.

 

3488854

 

captcha