IQNA

Tarjuma ya Kiamazigh ya Qur’ani yapongezwa nchini Morocco

19:51 - January 06, 2025
Habari ID: 3480010
IQNA - Wanaharakati wa Kiamazigh wamekaribisha mpango wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Morocco wa kutayarisha tarjuma ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kiamazigh. Jitihada za kukuza lugha ya Kiamazigh katika Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ni hatua muhimu na ya maana kuelekea kuamsha utambulisho rasmi wa Kiamazigh, alisema Abdullah Bu Shatart, mwanaharakati.

Alitoa wito kwa matumizi mapana ya lugha ya Kiamazigh katika programu za wizara na kwa maimamu na wahubiri wa misikiti, ndani na nje ya Morocco, ili kuwa na ujuzi wa lugha hii kwa ajili ya kuwezesha mwingiliano na wananchi na wachache katika nchi hiyo, iliripoti tovuti ya Sawt al-Maghrib.  

Tarjuma ya Qur’ani kwa lugha ya Kiamazigh ni hatua muhimu kwa lugha na utamaduni wake, alisema. Hapo awali, Hussein Jahadi al-Ba’amrani, mtafiti wa Morocco, alichapisha tafsiri ya kwanza ya Qur’ani kwa lugha ya Kiamazigh mwaka 2003. Alijitolea juhudi kubwa kwa mradi huu, na utafiti, uhariri, na tafsiri ya kazi hii ilichukua miaka 12 kukamilika. Pia, Imad Al-Mounyari, rais wa Jumuiya ya Utafiti na Mabadilishano ya Utamaduni ya Morocco, alisema, “Tunazingatia mpango wa wizara ya wakfu wa kutafsiri Qur’ani kwa lugha ya Kiamazigh kuwa hatua chanya inayounda mazingira ya kupata tafsiri rasmi ya Qur’ani kwa lugha hii.” Aliongeza kuwa tafsiri ya al-Ba’amrani ya Qur’ani na vitabu vya Kiislamu inaweza kutumika kama msingi wa tafsiri mpya. Kiamazigh imekuwa lugha rasmi nchini Morocco tangu mwaka 2011. Kulingana na takwimu rasmi, karibu theluthi moja ya idadi ya watu wa Morocco milioni 35 wanaweza kuzungumza lugha hiyo.

3491339

Kishikizo: qurani tukufu Amazigh
captcha