IQNA

Maqari wa Misri Kushiriki katika vikao vya  Qur'ani mwezi wa Ramadhani 

21:43 - February 16, 2025
Habari ID: 3480229
IQNA – Wizara ya Wakfu ya Misri inapanga kufanya programu mbalimbali za Qur'ani na kidini wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Maqari wa Misri Kushiriki katika vikao vya  Qur'ani mwezi wa Ramadhani Zinajumuisha usomaji wa Qur'ani, Sala za Taraweeh, mabaraza, usomaji wa vitabu kuhusu Seerah ya Mtume Mtukufu (SAW) na programu maalum kwa watoto. 

Maqari maarufu wa nchi hiyo watashiriki kikamilifu katika programu za Qur'ani zitakazofanyika kwenye misikiti.

Idara ya Masuala ya Misikiti ya wizara hiyo imesema itakuwa ikiandaa matukio hayo kwa ushirikiano na Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar na mashirika kadhaa yanayohusiana. 

Ahmed Ahmed Nuaina, Abdul Nasir Hark, Ahmed Tamim al-Maraghi, Ahmed Awaz Abu Fuyuz, Sayid Abdul Karim al-Qaytani, Abdul Fattah al-Taruti na Taha al-Numani ni miongoni mwa maqari wakuu wanaotarajiwa kushiriki katika programu hizo katika Msikiti wa Imam Hussein (AS) katika mji mkuu Cairo. 

Mwezi wa Ramadhani mwaka huu unatarajiwa kuanza jioni ya Ijumaa, Februari 28, na siku ya kwanza ya kufunga kuwa Machi 1 na kuisha jioni ya Jumapili, Machi 30. 

Ramadan ni mwezi wa tisa na mtukufu zaidi wa kalenda ya Kiislamu, ambapo Waislamu wanakumbuka Wahyi wa Qur'ani kwa Mtume Muhammad (SAW). 

Wakati wa Ramadan, Waislamu wanafunga kutoka alfajiri hadi magharibi, kujiepusha na kula, kunywa, kuvuta sigara na uhusiano wa kijinsia na mengine yote yaliyokatazwa katika mchana wa mwezi huu mtukufu.. Pia wanatumia muda zaidi kwa swala, dua, dhikri, kutoa sadaka na kukithirisha matendo mema, wakitafuta kuimarisha imani yao na kutakasa nafsi zao. 

Moja ya mazoea ya Mwezi Mtukufu Ramadhani ni kusoma na kujifunza tafsiri ya Qur'ani. Waislamu hulenga kukamilisha usomaji wa Qur'ani yote mwishoni mwa mwezi.

3491872

captcha