IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Misikiti Misri inajiandaa kwa ajili ya Sala, Itikafu katika Mwezi wa Ramadhani

18:39 - March 06, 2023
Habari ID: 3476668
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Wakfu nchini Misri Sheikh Muhammad Mukhtar Jumaa alisema misikiti nchini humo iko tayari kuwapokea waumini ajili ya Sala za kila siku na ibada nyinginezo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Ibada hizo ni pamoja na sala za Taraweeh na Tahajjud na halikadhalika Itikakfu.

Zaidi ya misikiti 11,000 itafunguliwa kwa ajili ya Sala ya Tahajjud, na zaidi ya 6,000 kwa ajili ya Itikafu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Misri.

Tahajjud, ambayo pia inajulikana kama "Sala ya usiku," ni sala ya hiari na sio moja ya sala tano za faradhi ambazo Waislamu wanapaswa kusali kila siku.

Itikafu ni desturi ya Kiislamu ya kipindi cha kukaa msikitini kwa idadi fulani ya siku wakati wa Mwezi MtukufuRamadhani, kujishughulisha na ibada na kujiepusha na mambo ya kidunia. Vizuizi vya Corona vilizuia itikaf mwaka jana.

Kampeni ya kusafisha misikiti pia imezinduliwa na wizara hiyo ili kuandaa misikiti kwa ajili ya Ramadhani.

Hisham Abdel Aziz Ali, afisa wa wizara, aliongoza kampeni ya kusafisha Msikiti wa Sayyidah Nafisa wa Cairo.

Abdel Aziz alisema misikiti lazima iwe kielelezo cha usafi na uzuri, na kudumisha usafi na utakaso ni njia ya Mtume Muhammad Muhammad SAW na wafuasi wake.  

3482714

Habari zinazohusiana
captcha