IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Taa aina ya Fanous zauzwa kwa wingi Misri kabla ya Ramadhani

20:46 - March 08, 2024
Habari ID: 3478470
IQNA – Fanous (taa) imekuwa ishara ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika baadhi ya nchi kwa mamia ya miaka. Taa hii pia ni maarufu kama Fanous Ramadhan.

Nchini Misri, taa za kitamaduni za zinazotegnenezwa kwa mabati na kioo huwa ni miongoni mwa vifaa vinavyohitajika sana kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika soko la zamani huko Cairo, wafanya biashara huuza taa za kila aina kabla  kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Siku chache kabla ya mwezi mtakatifu, Wamisri huwa na ada na desturi ya kupamba nyumba zao na mitaa kwa taa za rangi. Mwezi wa Ramadhani (ambao huenda ikaanza Machi 12 mwaka huu) ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu. Qur'ani Tukufu iliteremshwa kwenye moyo wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) katika mwezi huu. Mwezi huu mtukufu ni kipindi cha kukithirisha sala, saumu, utoaji wa sadaka na uwajibikaji kwa Waislamu duniani kote.

Wakati wa Ramadhani, Waislamu hufunga (kujiepusha na vyakula na vinywaji na yote yaliyokatazwa) kuanzia wakati wa kabla ya Sala ya Afajiri hadi Magharibi.

3487464

Habari zinazohusiana
captcha