Kulingana na shirika la habari la Wafa, vikosi hivyo vilifanya upekuzi nyumbani kwake na kumhoji kiongozi huyo wa Kiislamu
Pia walibandika mlangoni mwake waraka wa kumtaka kufika kwenye kikao cha kusikilizwa kuhusu suala la kufukuzwa kwake.
Mnamo Agosti mwaka jana, baada ya Sheikh Sabri kuongoza dua kwa ajili ya aliyekuwa kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyah, na kutoa rambirambi kufuatia kifo chake, vikosi vya utawala wa Israeli vilimkamata na baadaye kumwachilia huku vikimzuia kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa.
Sheikh Sabri ni mkosoaji mkubwa wa uvamizi wa Israeli katika maeneo ya Palestina ambao umedumu kwa miongo kadhaa. Hapo awali, aliwahi kushikilia nafasi ya Mufti wa al-Quds na maeneo ya Palestina kuanzia mwaka 1994 hadi 2006.
Wakati huo huo, katika siku ya 30 ya uvamizi wa Israeli katika maeneo ya kaskazini ya Ukingo wa Magharibi, vikosi vya utawala haramu wa Israeli viliishambulia sehemu za Tulkarm, Nablus, na Al-Khalil.
Kijana mmoja wa Kipalestina alijeruhiwa katika mji wa Bita, kusini mwa Nablus, kutokana na mashambulizi ya vikosi vya uvamizi.
Vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel pia vilivamia Bait Rima, kaskazini-magharibi mwa Ramallah, na kuwakamata Wapalestina kadhaa.
Wakati wa uvamizi huo, mapigano makali yalizuka kati ya vikosi vya Kizayuni na Wapalestina.
3491927