"Usiku wa jana, tulikaribisha mkusanyiko wa mabalozi kutoka nchi za Kiislamu wanaoishi Tehran kwa chakula cha iftar," aliandika kwenye chapisho la mitandao ya kijamii Jumanne.
"Ilikuwa fursa ya kujadili upanuzi wa mahusiano ya kidiplomasia, kuimarisha ushirikiano wa pande kadhaa, na kuongeza kina cha mahusiano ya kitamaduni na kidini miongoni mwa nchi za Kiislamu," alisema Araghchi.
"Changamoto za hivi karibuni na matukio katika eneo letu yanaonyesha wazi umuhimu wa umoja na mshikamano wa kina miongoni mwa nchi za Kiislamu wakati huu hatari," aliendelea kusema.
Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waislamu hufunga kula na kunywa mchana sambamba na kujizuia na yote yaliyokatazwa kisheria kuanzia Alfajiri hadi Magharibi na kisha baada ya hapo hujumuika pamoja kwa ajili ya kufungua saumu.
3492435