IQNA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran atuma salamu za Idul Fitr, atoa wito wa umoja wa Kiislamu

20:43 - March 30, 2025
Habari ID: 3480472
IQNA-Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametoa wito wa kuimarisha zaidi umoja na huruma miongoni mwa mataifa ya Kiislamu. Katika ujumbe wa pongezi kwa wenzake Waislamu kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul Fitr, inayoadhimisha baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani,

Araqchi ametoa wito huo katika ujumbe wa pongezi kwa wenzake Waislamu kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul Fitr, inayoadhimisha baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Araghchi ameandika katika ujumbe wake siku ya Jumapili kwamba: “Ninatoa pongezi zangu za dhati kwa watu wa Iran pamoja na serikali na mataifa ya Kiislamu kwa mnasaba wa Idul Fitr. Nchini Iran, mwezi mtukufu wa Ramadhani – chemchemi ya Qur’ani – mwaka huu umeambatana na Nowruz (mwaka mpya wa Kiirani) na msimu wa machipuo wa maumbile."

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran amewaombea wanaume, wanawake na watoto wasio na hatia walioko Palestina, Lebanon na Yemen, ambao walikumbwa na mashambulizi ya kinyama na uhalifu uliotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

“Katika siku hii tukufu, namuomba Mwenyezi Mungu kwa dhati atupe umoja na huruma miongoni mwa mataifa ya Kiislamu kuliko wakati wowote ule,” amesema Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Iran.

4274289

captcha