IQNA

Mwanaharakati: Chuki dhidi ya Uislamu si tatizo la Waislamu pekee, bali ni janga la dunia

13:18 - May 28, 2025
Habari ID: 3480753
IQNA – Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) ni janga la kimataifa linaloathiri jamii nzima, si Waislamu pekee, alionya Abdulsamad Al-Yazidi, Mwenyekiti wa Kituo cha Kiislamu cha Ujerumani.

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa uliofanyika Baku, wenye maudhui ya “Angazio la Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia): Kufichua Upendeleo, Kuvunja Madharau”, Al-Yazidi alisisitiza kwamba licha ya kuteuliwa kwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu chuki dhidi ya Uislamu kuwa hatua muhimu, bado haitoshi kukabiliana na ukubwa wa tatizo hili.

“Tatizo hili linapingana na kila kanuni ya utu na ubinadamu. Huko Ujerumani, kwa mfano, chuki ya wazi dhidi ya Waislamu huonyeshwa hata ndani ya bunge na wakati mwingine hupigiwa makofi , hakuna dini nyingine inayodhulumiwa kwa namna hiyo,” alisema.

Al-Yazidi amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya chuki na ubaguzi si jukumu la Waislamu peke yao.

“Mielekeo mikali barani Ulaya inazidi kuwa tishio, na jamii ya kimataifa inalazimika kushirikiana kwa pamoja kukabiliana na hatari hii,” aliongeza.

Aliendelea kueleza kwamba Islamophobia kwa makosa hutazamwa kama tatizo la Waislamu pekee, ilhali kwa uhalisia wake, huchochea mgawanyiko na machafuko ambayo huumiza jamii nzima.

“Mtazamo huu, pamoja na vitendo vya makundi yenye nia ya kuwagawa watu, hupelekea ghasia na upotevu wa maisha,” alihitimisha.

3493247

Habari zinazohusiana
captcha