IQNA

Kitabu Kipya cha Sayansi ya Qur’ani kutimika katika vyuo vya Kiislamu nchini Iran

16:59 - June 08, 2025
Habari ID: 3480806
IQNA – Kitabu kipya kilichoandikwa kuhusu sayansi ya Qur’ani kimetangazwa rasmi kama rasilimali ya elimu kwa wanafunzi wa kiwango cha kwanza katika vyuo vya Kiislamu kote Iran.

Kitabu hicho, kinachoitwa Ulum-ul Qur'an (Sayansi ya Qur’ani), kilizinduliwa katika hafla maalum siku ya Jumamosi, Juni 7. Mradi huu umeongozwa na Hujjatul -Islam Seyyed Reza Moaddab, ambaye pia ndiye mhariri mkuu wa kitabu hicho. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Moaddab alieleza kuwa kitabu hiki kimeandaliwa ili kuwazoeza wanafunzi wa vyuo vya Kiislamu katika mada muhimu za utangulizi zinazohusiana na uelewa wa Qur’ani. Mada hizo zinajumuisha miujiza ya Qur’ani, mchakato wa Wahy, ukusanyaji wa maandiko, na mbinu za tafsiri. 

“Kitabu hiki kimeandikwa kwa ushirikiano wa wanazuoni tisa mashuhuri kutoka chuo cha Kiislamu,” alisema Moaddab. “Hii inaweza kuchukuliwa kama moja ya juhudi za kwanza za pamoja katika uwanja huu, ikichukua mbinu ya kisasa inayozingatia mitazamo ya hivi karibuni ya kielimu na kitafsiri.” Alifafanua kuwa mchakato wa uandishi ulichukua takriban miaka miwili na nusu, na kila sehemu ya kitabu iliandikwa na mtaalamu wa mada husika.

Aliongeza: “Tumejitahidi pia kuingiza maoni ya watu mashuhuri kama Allamah Tabatabai. Bila shaka, hakuna kitabu kilicho huru na uboreshaji, na tunatarajia matoleo yajayo yatanufaika kutokana na maoni yatakayokusanywa wakati wa matumizi darasani.” 

Hujjatul Islam Farhad Abbasi, Naibu wa Utafiti katika Kituo cha Maendeleo ya Mtaala katika Chuo cha Kiislamu, pia alizungumza katika hafla hiyo. Alisisitiza umuhimu wa kitabu hicho, akisema: “Hiki kitakuwa chanzo rasmi cha kozi ya ‘Sayansi ya Qur’ani’, ambayo itajumuisha masomo ya saa 32 na itaingizwa kwenye mtaala wa vyuo vya Kiislamu kote nchini.” Aliangazia sifa kadhaa za kipekee za kitabu hicho, ikiwa ni pamoja na waandishi wake wa pamoja, maudhui yake yanayofafanua kwa kina, na ulinganifu wake na mbinu za kisasa za elimu.

“Pia kinatoa majibu bunifu kwa maswali ya kisasa na kinajumuisha matokeo ya hivi punde ya kitaaluma,” Abbasi aliongeza. Kitabu hicho kinatarajiwa kufundishwa katika zaidi ya vyuo 400 kote nchini.

3493365

captcha