IQNA

Hatua ya awali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani kwa wanafunzi wa Kiislamu Imeanza mtandaoni

18:27 - July 20, 2025
Habari ID: 3480970
IQNA-Hatua ya Awali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani kwa Wanafunzi wa Kiislamu Imeanza kwa Njia ya Mtandao

Hatua ya awali ya mashindano ya kimataifa kuhifadhi Qur’ani Tukufu kwa ukamilifu, katika awamu ya saba ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani kwa wanafunzi wa Kiislamu, imeanza kwa njia ya mtandao kupitia Kituo cha Qur’ani cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Vya Iran.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IQNA, mashindano haya yameanza leo Julai 19 kwa njia ya mtandao katika studio ya Mobin ya Shirika la Qur’ani la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, na yataendelea hadi tarehe 23 Julai.

Katika siku ya kwanza, washiriki kadhaa walijitokeza kupitia mawasiliano ya video ya moja kwa moja ili kuonyesha yale waliyoyahifadhi. Hatua hii ya mashindano inaendeshwa chini ya uamuzi wa jaji Ustadh Mu'taz Aghaei.

Kwa mujibu wa taarifa ya sekretarieti ya awamu ya saba ya mashindano haya, jumla ya washiriki 47 kutoka nchi mbalimbali wanashiriki katika hatua ya awali ya mashindano ya kuhifadhi Qur’ani kwa ukamilifu.

Aidha, wiki ijayo kutafanyika mtihani wa kuwachagua wawakilishi wa nchi yetu katika fani za qira’a ya tahqiq na kuhifadhi Qur’ani yote. Mtihani huo utafanyika kwa njia ya kutuma faili za video za usomaji wa washiriki kwa jopo la majaji.

4295239

Habari zinazohusiana
captcha