IQNA

Imam Hussein (AS) katika Qur'an /3

Faida za Imani ya Raj’a katika mwamko wa Imam Hussein (AS)

9:48 - July 05, 2025
Habari ID: 3480896
IQNA – Imani juu ya Raj’a (kurejea duniani) katika mwamko wa Imam Hussein (AS) pamoja na masahaba wake waaminifu, hubeba baraka nyingi za kiroho na maadili.

Katika tafsiri ya baadhi ya aya za Surah Al-Isra, kama vile aya ya 6:
Kisha tukakurudishieni nguvu zenu dhidi yao,...", Imam Sadiq (AS) amesema:

“Kudhihiri na kurejea kwa Imam Hussein (AS) kutafanyika akiwa na wafuasi wake sabini waaminifu, wakiwa wamevaa kofia za dhahabu. Watatokea kutoka pande mbili tofauti na watatangaza kwa watu kuwa huyu ni Hussein, ambaye amerudi na kuonekana tena, ili asiwepo muumini yeyote mwenye shaka. Hakutakuwa na mashaka kuwa yeye si Dajjal wala Shetani, na kwamba Hujjat ibn al-Hassan (Imam Mahdi), bado yupo miongoni mwa watu. Mara tu itakapothibitika mioyoni mwa waumini kuwa huyu kweli ni Hussein (AS), ndipo wakati wa kuaga dunia kwa Imam Mahdi (Allah aharakishe kudhihiri kwake) utakapowadia. Imam Hussein (AS) ndiye atakayemwosha, kumvisha sanda, kumpaka kafuri, na kumzika, kwa kuwa hakuna yeyote ila Mrithi (Wasi) na Imam anayeweza kuuosha mwili wa Wasi mwingine.”

Kuamini katika kurejea kwa Imam Hussein (AS) na masahaba wake waaminifu ni miongoni mwa misingi muhimu ya madhehebu ya Ahlul-Bayt (AS), na inazaa matunda makubwa ya kiroho na kimaadili.

Faida ya kwanza ya kiitikadi katika kuamini Raj’a ya Ahlul-Bayt (AS), hasa Imam Hussein (AS), ni kwamba inaonesha kuwa Imam (AS) na wafuasi wake hawakufunikwa na historia tu, bali msafara huu, unaoongozwa na mjukuu huyo wa Mtume Muhammad (SAW) bado unaendelea na utarejea tena katika zama za baadaye.

Faida ya pili ya kiakili ni kuwa muumini hupata yakini kwamba msafara huu bado upo hai, si wa watu waliokwisha kufa. Hivyo basi, kila wakati na kila mwaka, msafara huu huwapokea watu wa mioyo safi duniani, kitu kinachoonekana wazi kupitia mapenzi yasiyokoma kwa Imam Hussein (AS). Mkusanyiko wa Muharram na Arbaeen ni ushahidi wa ukweli huu.

Faida ya tatu ni kuwa imani hii huweka matumaini katika nyoyo za wapenzi wa Ahlul-Bayt (AS), na kuwafanya wawe na shauku ya kuungana na msafara wa Husseini. Tarajio hili huleta mageuzi katika namna jamii ya waumini wanavyoelewa matukio ya Karbala na Ashura, na hatimaye hurekebisha mienendo na maadili yetu.

Kwa maneno mengine, kadri waumini wanavyozidi kuamini kwa dhati ndani ya nyoyo zao kuwa Imam Hussein (AS) atarejea, ndivyo wanavyozidi kujitahidi kusafisha matendo yao. Kwa kujua kuwa Imam atarudi, hujitenga na tabia za maadui wa Ahlul-Bayt (AS) na kushikamana na maadili mema, ili pengine, siku moja, wahesabiwe miongoni mwa jeshi la Imam wakati wa kurejea kwake.

3493696

captcha