IQNA

Imam Hussein (AS) katika Qur'an /4

Raj’a ya Imam Hussein (AS): Muendelezo wa Nusra ya Mwenyezi Mungu kwa Manabii na Waumini

11:45 - July 06, 2025
Habari ID: 3480897
IQNA – Nusra ya Mwenyezi Mungu hujitokeza kwa namna mbalimbali kwa manabii wa Mwenyezi Mungu na waumini wa kweli.

Kwa kuwa Imam Hussein (AS) aliuawa kwa dhulma huko Karbala, basi nusra ya Mwenyezi Mungu inaendelea kupitia Raj’a yake (kurejea kwake duniani) kabla ya Siku ya Kiyama.

Katika siku ya Ashura, katika hotuba yake ya mwisho, Imam Hussein (AS) alitangaza:

“Mimi nitakuwa wa kwanza ambaye ardhi itapasuka kwa ajili yake, na nitadhihiri; kudhihiri huku kukiwa sambamba na kudhihiri kwa Amir al-Mu’minin (AS) [Imam Ali], kudhihiri kwa Qa’im wetu [Imam Mahdi anayesubiriwa (Allah aharakishe kudhihiri kwake)], na maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW).”

Imam Sadiq (AS) alisema:

“Wa kwanza ambaye kaburi litapasuka kwa ajili yake, na ambaye ataondosha mavumbi kichwani mwake, ni Hussein ibn Ali (AS). Atatokea pamoja na wafuasi elfu sabini na tano.”

Kisha alirejelea  aya mbili za Qur'ani:

"Hakika tutawanusuru Mitume wetu na wale walioamini katika maisha ya dunia, na Siku ambayo mashahidi watasimama, Siku ambayo udhuru wa madhalimu hautawafaa kitu, nao witalaaniwa, na watapata makaazi mabaya kabisa." (Surah Ghafir, aya 51-52)

Faida za Kuamini Raj’a ya Imam Hussein (AS)

Qur'an Tukufu huzungumzia mara kwa mara kuhusu nusra ya Mwenyezi Mungu kwa manabii na waumini. Hapa chini ni baadhi ya mifano:

 Nusra kwa Nuhu (AS): "Basi tukamuokoa yeye na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina." (Surah Ash-Shu’ara, aya 119)

Nusra kwa Ibrahim (AS): "Tukasema kwa moto: 'Uwe baridi na salama kwa Ibrahim.'" (Surah Al-Anbiya, aya 69)

Nusra kwa Lut (AS): "Na tulimuokoa yeye pamoja na watu wake wote, isipokuwa mke wake." (Surah Al-Hijr, aya 59)

Nusra kwa Yusuf (AS): "Na namna hiyo tukamweka Yusuf nchini, akaishi popote alipotaka." (Surah Yusuf, aya 56)

Nusra kwa Shu’ayb (AS): "Na tulipokuja amri yetu, tulimuokoa Shu’ayb kwa rehema yetu, pamoja na wale waliomuamini." (Surah Hud, aya 94)

Nusra kwa Salih (AS): " Basi ilipo kuja amri yetu tulimwokoa Saleh na wale walio amini pamoja naye kwa rehema yetu." (Surah Hud, aya 66)

Nusra kwa Hud (AS): "Ilipo fika amri yetu, tulimwokoa Hud na walio amini pamoja naye, kwa rehema itokayo kwetu." (Surah Hud, aya 58)

 

3493713

captcha