IQNA

Wanamichezo Waislamu

Nimerudi Nyumbani’: Bingwa wa Dunia Fred Kerley asema baada kuukumbatia Uislamu

18:53 - July 06, 2025
Habari ID: 3480906
IQNA – Nyota wa Marekani katika mchezo wa riadha, Fred Kerley, ametangaza kuingia katika Uislamu, akishiriki tukio hilo takatifu kupitia video aliyopakia kwenye Instagram.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye ameshinda medali kadhaa katika Mashindano ya Dunia ya Riadha na Michezo ya Olimpiki, alitamka shahada, tamkko la la imani ya Kiislamu, ndani ya msikiti.

Kupitia chapisho lake, Kerley aliwasambazia wafuasi wake video ya kipindi hicho cha kusilimu au kuingia kwake katika Uislamu. Katika maandishi aliyoweka, aliandika: “Walijaribu kunivunja, Allah akanijenga upya. Leo nimetamka shahada yangu. Mimi ni mteule. Nimelindwa. Nimerudi nyumbani.”

Kerley ameonesha mafanikio makubwa katika majukwaa ya kimataifa. Ana medali tatu za dhahabu, moja ya fedha, na moja ya shaba katika mashindano ya dunia. Katika Olimpiki za Tokyo 2020, alipata medali ya fedha kwenye mbio za mita 100 kwa wanaume, na hivi karibuni alipata shaba kwenye mbio hizo katika Olimpiki za Paris 2024.

4292719

captcha