IQNA

Misikiti ya Misri kufunguliwa tena kwa ajili ya Swala ya Ijumaa

13:04 - August 23, 2020
Habari ID: 3473094
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Wakfu nchini Misri Sheikh Mukhtar Gomaa, ameamuru kuazishwe kampeni ya kitaifa ya kutayarisha misikiti kote nchini kwa ajili ya Swala ya Ijumaa wiki hii.

Ametaka misikiti yote isafishwe kwa dawa za kuangamiza virusi na alama maalumu zichorwe kuanisha eneo la ambalo kila mtu atatumia wakati wa kuswali ili kuhakikisha kuwa kanuni ya kutokaribiana inazingatiwa.

Aidha amesema wafanyakazi wote wa misikiti wanapaswa kurejea kazini ili tayarisha misikiti kwa ajili ya kutayarisha misikiti.

Misikiti yote Misri ilisitisha swala za jamaa na ijumaa kuanzia Machi 21 ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Baadhi ya misikiti ilifunguliwa Juni 27 kwa ajili ya swala tano za kila siku lakini Swala ya Ijumaa bado ilikuwa ni marufuku.

Sheikh Gomaa amesema Swala ya Ijumaa itaswaliwa katika misikiti yote mikubwa na misikiti ya vyuo vikuu kuanzia Agosti 28. Aidha amesisitiza kuwa misikiti inapaswa kuzingatia kanuni kadhaa wakati wa swala za Ijumaa ambazo ni pamoja na waumini kutokaribiana, kuvaa barakoa, kila muumini kubeba zulia au mkeka binafsi wa kuswali, misikiti kufunguliwa dakika kumi kabla ya swala na kufungwa punde baada ya swala kumalizika, idadi maalumu ya waumini kwa kuzingatia ukubwa wa msikiti, hotuba zisizidi dakika 10, kutofungua vyoo, kutoswalia swala za janaza ndani ya misikiti na kufungwa haram takatifu au maziyara katika maeneo ya misikiti.

Waziri wa Wakfu Misri ameongeza kuwa wafanyakazi katika misikiti watakuwa na jukumu la kutekeleza sheria za kuzuia kuenea corona.

3472344

captcha