IQNA

Misaada kwa jamii

Shirika la misaada Kuwait lajenga Misikiti 30 katika nchi tofauti

16:32 - January 04, 2023
Habari ID: 3476355
TEHRAN (IQNA) – Mkurugenzi wa Taasisi ya Zakat al-Andalus inayohusiana na Jumuiya ya Hisani ya Al-Najat amesema jumuiya hiyo ya Kuwait imejenga misikiti 30 katika nchi tofauti za Kiislamu na Kiarabu mwaka jana.

Zaid al-Hameli alisema ujenzi na ukarabati wa misikiti ni moja ya shughuli kuu za jimuiya hiyo.

Alisema miradi ya ujenzi wa misikiti hiyo inafanywa katika nchi maskini ambazo watu wake wanahitaji maeneo zaidi ya ibada.

"Tunatumai kuigeuza misikiti hii ambayo imejengwa (na jumuiya) kuwa taa za kukuza (mafundisho ya Kiislamu), ufahamu na utamaduni," alisema.

Al-Hameli ameongeza kuwa, duru za Qur'ani, Iftar na matukio yanayosaidia kustawisha utamaduni wa Kiislamu ni miongoni mwa shughuli zinazofanywa katika misikiti hiyo.

Al-Najat Charity Society ni taasisi kuu ya kutoa misaada nchini Kuwait ambayo imekuza shughuli zake za Kurani na kidini katika miaka ya hivi karibuni.

Kufanya kozi za kufundisha Qur'ani mtandaoni kwa watoto na vijana na kuandaa programu za Qur'ani misikitini ni miongoni mwa shughuli zake.

4112138

Kishikizo: kuwait uislamu misikiti
captcha