IQNA

Misikiti Misri yarejea katika hali ya kawaida kabla ya corona

19:15 - May 07, 2022
Habari ID: 3475218
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu ya Misri imesema misikiti na maeneo yote ya ibada nchini humo yanaweza kuanza tena shughuli za kawaida kama ilivyokuwa kama ya janga la corona.

Katika agizo jipya, misikiti kote Misri itarejea katika hali ya kawaida ya ibada ambapo pia kutakuwa na darsa za Qur'ani, mihadhara ya kidini na ziara katika maeneo matakatifu bila vizingiti.

Msikiti Mtakatifu wa Imam Hussein AS pia utakuwa wazi kwa waumini nyakati zote za siku. Halikadhalika kumbi za sala za wanawake nazo pia sasa zitafunguliwa baada ya kufungwa kwa miaka miwili.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Waziri wa Wakfu Sheikh Mokhtar Gomaa kuwasilisha mapendekezo kwa wizara ya mambo ya ndani kufuatia kupungua maambukizi ya corona nchini Misri.

  4054941

Kishikizo: misri Wakfu misikiti gomaa
captcha