Katika ujumbe rasmi aliomtumia Abdul Malik Badr al-Din al-Houthi, kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, Sheikh Qassem ametoa pole kwa taifa hilo na kulaani vikali hujuma hiyo ya kijeshi.
Amesisitiza kuwa mashambulizi ya Israel ni ishara ya kushindwa kwa adui, ukatili wa hali ya juu, na mauaji yasiyo na huruma dhidi ya binadamu. Kiongozi huyo wa Hizbullah ameongeza kuwa adui alitekeleza hujuma hiyo kwa sababu hawezi kukabiliana na majeshi ya Yemen na viongozi wake jasiri katika medani ya vita.
Mashambulizi hayo ya anga yaliyofanyika Alhamisi, Agosti 28, yalisababisha vifo vya viongozi wa juu wa serikali ya Yemen, wakiwemo mawaziri waliokuwa wakihudhuria warsha mjini Sanaa. Tukio hili linaashiria ongezeko kubwa la hujuma za kijeshi za Israel dhidi ya Yemen.
Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, harakati ya Ansarullah imethibitisha kuwa Waziri Mkuu Al-Rahawi na wanachama wengine wa serikali walilengwa moja kwa moja wakati wa warsha hiyo.
Akizungumza kupitia ujumbe wa video, Mahdi al-Mashat, mwanasiasa na afisa wa kijeshi wa Yemen, amesema: “Tutachukua kisasi, na tutaibua ushindi kutoka kwa majeraha yetu.”
3494436