IQNA

16:28 - January 25, 2021
News ID: 3473589
TEHRAN (IQNA) – Idara ya Masuala ya Kidini Uturuki (Diyanet) imewatunuku Waislamu wa Argentina vitabu 7,000 vya kidini na nakala za Qur'ani Tukufu zilizotarjumiwa kwa Kihispania.

Kwa mujibu wa taarifa, vitabu hivyo vilitunukiwa Kituo cha Kiislamu cha Argentina katika hafla iliyofanyika baada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Ahmad mjini Buenos Aires.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Balozi wa Uturuki nchini Argentina, Mkuu wa Kituo cha Kiislamu Argentina na Mkurugenzi Mkuu wa Diyanet.

Vitabu hivyo vinajumuisha tarjuma ya Qur'ani kwa lugha ya Kihispania, vitabu vya kufunza Qur'ani na pia kadi 40,000 zenye Hadithi za Mtume Muhammad SAW.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2010 za shirika la PEW, kuna Waislamu milioni moja kati ya watu wote milioni 44 nchini Argentina.

3949618

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: