IQNA

Mmarekani mfeministi aliyesilimu

Uhusiano na Mwenyezi Mungu ulinivutia katika Uislamu + Video

10:03 - November 15, 2021
Habari ID: 3474559
TEHRAN (IQNA)- Theresa Corbin aliwahi kuwa mfeministi sugu nchini Marekani lakini baada ya kupata nuru ya uwongofu, aliondoka katika Ukristo na kusilimu na sasa anazungumzo kuhusu yaliyomvutia katika Uislamu.

Bi. Corbin anasema: "Baada ya kusilimu, niliweza kubaini kuwa Uislamu si utamaduni au pote linalodhibiti eneo moja la dunia. Ilinibainikia kuwa Uislamu ni dini ya dunia ambayo inafunza kuhusu udugu, kuheshimiana, subira, stara, na msimamo wa wastani."

Aidha anazungumza kuhusu nukta muhimu iliyomvutia katika Uislamu na kusema: "Uhusiano na Mwenyezi Mungu mara tano kwa siku ni nukta iliyonivutia katika Uislamu." Pia anasema staha, hijabu na heshima aliyonayo mwanamke ni nukta nyingine iliyomvutia katika Uislamu.

4013183

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha