Mei 12, iliadhimishwa kuwa ni kumbukumbu ya kifo cha Sheikh al-Zamil. Alikuwa mmoja wa wasomaji maarufu wa Qur’ani Tukufu nchini Misri na katika ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.
Alizaliwa tarehe 22 Desemba 1929 katika kijiji kilicho karibu na jiji la Mansuriya, katika Mkoa wa Dakahlia, nchini Misri.
Watu kadhaa katika familia yake walikuwa watu wa dini na wenye kujishughulisha na Qur'ani Tukufu. Baba yake, Sheikh Mahmoud Mahmoud al-Zamil, alikuwa imamu wa kijiji hicho, mjomba wake wa upande wa baba alikuwa mhitimu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar na hakimu katika jiji la Mansuriya, na mjomba wake wa upande wa mama, Sheikh Mustafa Ibrahim, alikuwa ni hafidh wa Qur’ani yote.
Mjomba wake huyo wa mama ndiye aliyemhamasisha Sheikh Hamdi kuanza kuhifadhi Qur’ani akiwa bado mdogo.
Baada ya kuikamilisha hifdhi ya Qur'ani, Sheikh Hamdi alianza kujifunza tajwidi na mbinu za usomaji wa Qur’ani chini ya Sheikh Tawfiq Abdul Aziz, mtaalamu wa elimu za Qur’ani.
Baadaye alikua mmoja wa maqari mashuhuri nchini Misri. Alikuwa akisoma Qur'ani katika Redio ya Qur'ani ya Misri katika hafla na matukio mbalimbali kuanzia mwaka 1976 hadi kifo chake.
Alikuwa na mapenzi makubwa kwa qira’a za Sheikh Muhammad Rif’at, Mohamed Salamah, Ali Mahmoud, na Abdul Fattah al-Shaashaei.
Hata hivyo, alivutiwa zaidi na kuathiriwa sana na mtindo wa usomaji wa Sheikh Mustafa Ismail. Sheikh Hamdi al-Zamil alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kisukari akiwa na umri wa miaka 53, mnamo tarehe 12 Mei 1982.
Ifuatayo ni qira’a yake ya Aya za 111 hadi 117 za Surah At-Tawbah: