IQNA

Misri yamnyonga mwalimu wa Qur’rani aliyekuwa na umri wa miaka 80

16:07 - April 28, 2021
Habari ID: 3473856
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa kiimla nchini Misri umetekeleza hukumu ya kunyongwa dhidi ya wafungwa 18, akiwemo Sheikh Abdel Halim Jibrel, mwalimu wa Qur’ani aliyekuwa na umri wa miaka 80.

Wafungwa hao walihukumiwa kunyongwa mapema wiki baada ya mahakama kudai kuwa walihusika katika hujuma dhidi ya kituo cha polisi.

Wafungwa wengine ambao hukumu ya kunyongwa imetekelelzwa dhidi yao ni Walid Saad Abu Omaira, Mohamed Rizk Abuel Soud, Ashraf Sayed Rizk, Ahmed Owes Hussein, Essam Abdel Moety, Ahmed Abdel Nabi, Badr Abdel Nabi, Qutb Sayed Qutb, Omar Mohamed El-Sayed, Izzat Al-Attar, Ali El-Sayed Kenawy, Abdullah Saeed, Mohamed Yousef Al-Seidi, Ahmed Abdel Salam, Arafat Abdel Latif, Mustafa El-Sayed El-Kerfesh. Hukumu hiyo hiyo ilitekelezwa Aprili 26 katika Gereza la Wadi el-Natrun na familia za wafungwa hao zimetakiwa kwenda kuchukua maiti zao. 

Wote hao wanatuhumiwa kuua maafisa 13 wa polisi katika hujuma dhidi ya kituo cha polisi katika mtaa wa Kerdasa eneo la Giza mwaka 2013.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limelaani vikali hukumu hiyo na kusema haikizuingatia haki na uadilifu. Aidha Amnesty International imeulaani utawala wa Misri kwa kutekeleza hukumu hiyo bila huruma katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3474573

Kishikizo: misri
captcha