IQNA

Sanaa ya Qur'ani Tukufu

Kongamano la Orthografia ya Qur’ani nchini Libya

7:45 - October 18, 2022
Habari ID: 3475949
TEHRAN (IQNA) - Kongamano la kimataifa kuhusu orthografia wa Qur'ani limezinduliwa katika mji mkuu wa Libya wa Tripoli siku ya Jumatatu.

Wataalamu kadhaa na wanakaligrafia wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali watashiriki katika mkutano huo.

Kongamano ambalo  linatarajiwa kuendelea hadi Oktoba 19 limeandaliwa na Taasisi ya Qur'ani Tukufu ya Libya pembezoni mwa maonyesho ya maandishi ya Qur'ani.

Aidha kutakuwa na warsha kuhusu kaligrafia ya Qur'ani na sherehe za kuwaenzi washindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.

Wanakaligrafia kutoka nchi mbalimbali kama vile Misri, Algeria, Syria, Iraq, Mauritania, Oman, Morocco, Jordan, Palestina, Uturuki, Yemen na Saudi Arabia wanaonyesha kazi zao za sanaa za Qur'ani kwenye maonyesho hayo.

Miongoni mwao pia mwakilishi wa Iran Omid Rabbani, ambaye ni Ustadhi bingwa wa Kaligrafia na mwanachama wa Jumuiya ya Kaligrafia ya Iran.

Idadi kadhaa ya Misahafu iliyoandikwa kwa maandishi tofauti ya kaligrafia pia itaonyeshwa kwenye maonyesho hayo.

 

4092173

captcha