IQNA

Usajili wa Mashindano ya Qur’an Nchini Misri Waaanza

14:07 - December 20, 2025
Habari ID: 3481685
Mashindano haya yatafanyika katika kipengele cha kuhifadhi Qur’an kwa wanafunzi wa kiume na wa kike kutoka vituo vya mafunzo ya kuhifadhi Qur’an kote Misri.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, mashindano yamepangwa ndani ya mkakati wa wizara wa kuendeleza, kuimarisha ufahamu sahihi wa maana na madhumuni ya Qur'ani Tukufu.

Kila kituo kitachagua wanafunzi bora watano wa kiume na watano wa kike, waliotangazwa na wakuu wa vituo vya mafunzo ya kuhifadhi Qur’an, kushiriki katika mashindano haya, mradi tu hawajawahi kushiriki katika matoleo yaliyopita.

Wale watakaoshindwa kutimiza masharti muhimu katika hatua yoyote ya mashindano wataondolewa, imesema taarifa hiyo.

Mwisho wa kuwasilisha barua za utambulisho kwa Idara Kuu ya Masuala ya Qur’an ya wizara ni tarehe 31 Disemba 2025.

Kuhusu zawadi, wizara imepanga zawadi za pauni za Kimasri 70,000, 50,000 na 30,000 kwa washindi wa nafasi ya kwanza hadi ya tatu mtawalia. Zawadi hizi zitakabidhiwa kwa kituo husika na kugawanywa kati ya wanafunzi bora, mkuu wa kituo na maafisa wa Qur’an wa eneo hilo.

Aidha, imeamuliwa kuwa mshiriki yeyote atakayepata alama ya asilimia 80 au zaidi katika mashindano kati ya vituo viwili atapewa zawadi ya pauni 2,000.

Wizara iliongeza kuwa mashindano haya yatafanyika katika Msikiti wa Al-Rahma jijini Cairo.

3495786

captcha