IQNA

Misri kuanda mashindano ya Qur'ani Bandari ya Port Said

16:51 - December 17, 2021
Habari ID: 3474685
TEHRAN (IQNA)- Wakuu wa Jimbo la Port Said nchini Misri wametangaza mpango wa kuandaa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Port Said mwakani.

Gavana wa Port Said Abdel Mohammad Ibrahim Yousef al Ghadhban amesema mkutano umefanyika hivi karibuni kwa ajili ya kuandaa mashindano hayo na kusema kikao hicho kimehudhuriwa na wakuu wa Idara ya Wakfu na Chuo cha Al Azhar.

Amesisitiza kuhusu umuhimu wa mashindano ya Qur'ani ambayo huwa na wawakilishi kutoka mataifa mbali mbali na kuongeza kuwa mashindano hayo yanaashiria ustaarabu na utamaduni wa Misri.

Al Ghadhban amesema mashindano hayo yanalenga kuinua kiwango cha uelewa wa Qur'ani miongoni mwa vijana.

Mashindano ya Tano ya  Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Port Said yanatazamiwa kufanyika Februari 2020.

Alhamisi kulifanyika sherehe za kufunga rasmi Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Misri yaliyofanyika mjini Cairo. Mashindano hayo yalikuwa na washiriki 74 kutoka nchi mbali mbali walioshiriki katika mashindano ambayo mwaka huu yamepewa jina la qarii mashuhuri wa Misri Muhammad Sidiq Minshawi.

4018931

captcha