IQNA

Harakati za Palestina za Hamas na Jihad Islami zalaani Dkt. Larijani

12:15 - March 19, 2026
Habari ID: 3482071
IQNA-Harakati za Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) Palestina zimelaani mauaji ya afisa mkuu wa usalama wa Iran, Ali Larijani, na kuahidi kuendeleza njia na msimamo wake.

Harakati za Hamas na Jihad Islami zimetuma salamu zao za rambirambi za dhati kufuatia kuuawa kwa Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran Dkt. Ali Larijani, pamoja na mwanawe, katika shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano, Hamas imewasilisha salamu zake za rambirambi  kwa uongozi na wananchi wa Iran kufuatia kifo cha Larijani, mwanawe, na baadhi ya wenzake waliouawa katika shambulio la mabomu la Israel dhidi ya mji mkuu wa Iran, Tehran, tukio lililotajwa kuwa ni uvamizi wa wazi.

Taarifa hiyo imesema: “Tunaendelea kuthibitisha mshikamano wetu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo kwa sasa inakabiliwa na mashambulizi ya muungano wa Kizayuni na Marekani. Kuendelea kwa mashambulizi haya ni uhalifu unaolenga eneo lote la Asia Magharibi na unatishia usalama na uthabiti wake. Utawala wa Marekani pamoja na utawala ghasibu wa Israel wenye mielekeo ya kifashisti wanabeba dhima ya hatari zitakazotokana na hatua hizi.”

Hamas  imemuomboleza Shahidi Larijani na mashahidi wote waliouawa katika mashambulizi hayo, ikikumbusha mchango wake katika kuunga mkono kadhia ya Palestina na haki halali za watu wa Palestina.

Hamas imesema: “Tunamkumbuka kwa heshima kubwa misimamo yake ya heshima katika kuunga mkono kadhia ya Palestina na haki za watu wetu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amfunike kwa rehema zake pana, awape familia yake na ndugu zake subira njema na ustahimilivu, na awahifadhi watu wa Iran dhidi ya kila madhara na shari,” Hamas ilisema.

Kwa upande mwingine, harakati ya Jihad Islami ya Palestina pia ilitoa rambirambi zake za dhati kwa uongozi, serikali, na wananchi wa Iran kufuatia kuuawa shahidi Dkt Larijani, pamoja na Kamanda wa vikosi vya kujitolea vya Basij, Meja Jenerali Gholamreza Soleimani, na wenzao waliouawa katika shambulio la kigaidi la Israel dhidi ya Tehran.

Katika taarifa yake, harakati hiyo ilisema:

“Tumemfahamu shahidi Larijani na ndugu zake miongoni mwa makamanda waliouawa kuwa watetezi wa kweli wa Palestina na kadhia yake, na pia wafuasi thabiti wa watu wetu na mapambano yao katika majukwaa yote ya Muqawama kwa njia mbalimbali.”

Jihad Islami imeongezaz kuwa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu hayatapunguza azma ya wananchi wa Iran, bali yataongeza uthabiti wao katika kulinda nchi yao, uhuru wao, na mamlaka yao ya kitaifa dhidi ya mipango ya kidhalimu ya mabeberu.”

3496815

Kishikizo: larijani shahidi
captcha