
Sekretarieti ya baraza hilo imetoa taarifa rasmi kuthibitisha kuwa Larijani ameuawa shahidi Jumanne katika hujuma hiyo ya kigaidi. Ifuatayo ni matini ya taarifa hiyo.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
“Miongoni mwa Waumini wapo wanaume waliotimiza kwa uaminifu ahadi yao kwa Mwenyezi Mungu. Wapo waliokwisha kutekeleza nadhiri yao, na wapo wanaosubiri; wala hawakubadilisha msimamo wao hata kidogo.”
Kwa taifa tukufu na lenye fahari la la Iran:
“Mja wa Mungu amerejea kwa Mola wake.”
Roho safi za mashahidi zimempokea mja mwema wa Mwenyezi Mungu, Shahidi Dkt. Ali Larijani. Baada ya maisha marefu ya kujitolea na jihadi kwa ajili ya kuinua heshima ya Iran na Mapinduzi ya Kiislamu, hatimaye amefikia tamanio lake la muda mrefu. Ameitikia wito wa Mola wake na kupata kwa heshima kubwa daraja la shahada akiwa katika safu ya huduma kwa taifa.
Sasa ameungana na Imam wa mashahidi wa Ramadhani, Amiri wa Waumini Imam Ali (amani iwe juu yake); pamoja na kiongozi wa msafara wa mapambano na juhudi dhidi ya Marekani na Israel, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei; mwalimu wake shahidi Ayatullah Morteza Motahhari; na wenzake waliotangulia katika shahada, Sayyid Hassan Nasrallah na Haj Qassem Soleimani.
Hadi dakika za mwisho za maisha yake yenye baraka, aliendelea kujitahidi kuinua neno la Mwenyezi Mungu na kusimamia kwa bidii heshima na maendeleo ya Iran azizi. Daima aliwahimiza wananchi na viongozi kudumisha mshikamano na umoja mbele ya adui mwenye ukatili.
Katika alfajiri ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, yeye pamoja na mwanawe mwaminifu Mortaza, naibu wa usalama wa sekretarieti ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa Alireza Bayat, pamoja na walinzi kadhaa jasiri, walipata daraja tukufu la shahada.
Ushindi wa hakika unawasubiri wale wanaopigania njia ya haki. Mashahidi hawa watazidisha azma ya taifa na ya umma kuendeleza njia ya watu hao wa Mungu.
Kufa kwake shahidi ni tukio la baraka kwani miaka yake mingi ya jitihada na kujitolea hakustahiki kingine isipokuwa fahari hii aliyopata
Kumbukumbu yake idumu milele, na njia yake ifuatwe na wengi.
“Basi tukawalipiza kisasi wale waliotenda uhalifu, na ni haki juu Yetu kuwapa ushindi Waumini.”
Sekretarieti ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa
17/03/2026
3496803