IQNA

Turathi ya Kiislamu

Msomi wa Kimisri ana Msahafu wa Sentimita 3 ya Qur'ani ulioandikwa miaka 280 Iliyopita

18:56 - December 22, 2023
Habari ID: 3478074
IQNA - Profesa wa jiografia wa Misri ana nakala ndogo sana ya Qur’ani Tukufu (Msahafu) ambayo ni ya miaka 280 iliyopita.

Sayed Ahmed Qassim, ambaye anafundisha jiografia katika Chuo Kikuu cha Asyut, alisema bibi (nyanya) yake alimpa nakala hiyo miaka 50 iliyopita.

Alikuwa amerithi kutoka kwa baba yake, alisema, kulingana na jarida la Al-Watan. Kila ukurasa wa nakala una urefu wa sentimita tatu tu.

Ahmed anasema tarehe ya kuchapishwa imechapishwa kwenye jalada la nakala.

Msahafu huu mdogo ulichapishwa nchini Uturuki wakati wa utawala wa Uthmaniya  (Ottoman), anasema, akibainisha kuwa nakala hiyo inatunzwa katika kasha ndogo.

Kioo cha kukuza kinahitajika ili kusoma aya kwa sababu maneno ni madogo sana.

Mara nyingi watu hutembelea nyumba yake kuona na kusoma nakala hiyo ndogo na ya kale ya Qur’ani Tukufu, Ahmed anasema.

Anasisitiza kwamba hajawahi kufikiria kuuza nakala hiyo ya thamani ya Qur’ani Tukufu kwa sababu anataka kumpa mmoja wa watoto wake.

  4188575

Habari zinazohusiana
captcha