Maktaba hiyo ilizindua Jumanne Msahafu huo ulioandikwa na Ali Naghi Al-Isfahani mnamo mwaka wa 1266 Hijiria.
Nakala hii ya thamani ilitolewa kwa Mohammad Javad Azadeh na marehemu baba yake Haj Mehdi Azadeh mwaka wa 1960, kusherehekea kuhitimu kwake kutoka Kitivo cha Tiba katika Chuo Kikuu cha Isfahan. Katika barua moja, baba alimhimiza mwana huyo kutanguliza kuwatendea wema maskini bila kutayarajia malipo ya kidunia.
Baada ya miaka ya kuutunza Msahafui huo wa kipekee, familia ya Azadeh iliamua kuuzawadia taasisi ya umma.
"Msahafu huu una thamani kubwa na umuhimu wake ni mkubwa zaidi wakati wengine wanapopata fursa wa kunufaika nao," Majid Azadeh alisema katika hafla ya uzinduzi.
"Ndiyo maana tuliamua kuukabidhi kwa Maktaba Kuu ya Chuo Kikuu cha Tehran, sambamba na msisitizo wa babu yangu juu ya utamaduni wa hisani," aliongeza.
Wasemaji wengine pia walipongeza mchango wa familia pamoja na uzuri wa hati hiyo.
Fatemeh Saqafi, mkurugenzi wa maktaba, aliishukuru familia ya Azadeh kwa kutoa Msahafu huo.
3489230