iqna

IQNA

IQNA- Waislamu zaidi ya milioni 20 wamekusanyika Karbala nchini Iraq kwa ajili ya Arubaini ya mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS.
Habari ID: 3470688    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/11/21

Sayyid Hassan Nasrallah
Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, amesema anaitazama itikadi ya misimamo mikali ya Uwahhabi kuwa hatari zaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3470581    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/09/27

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia umuhimu wa umoja katika Ulimwengu wa Kiislamu na kusema kuwa, kuchochea makundi mengine ya Kiislamu kwa jina la Ushia kimsingi ni Ushia unaofadhiliwa na Uingereza.
Habari ID: 3470573    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/09/20

Sheikhe Mkuu wa Al Azhar
Sheikh Ahmed el-Tayyib, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar, Misri ametoa wito kwa maulmaa wa Shia na Sunni kutoa fatwa ambazo zitawazuia Waislamu wa madhehebu hizo kusitisha malumbano ya kimadhehebu.
Habari ID: 3470474    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/26

Wanazuoni wa Kishia nchini Misri wamepongeza Chuo Kikuu cha Al Azhar kwa hatua yake ya kuasisi kituo cha kukurubuisha madhehebu ya Kiislamu.
Habari ID: 3470311    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/14

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia atahadharisha
Russia imetahadharisha kuwa mgogoro was asa nchini Syria huenda ukaibua mgawanyiko mkubwa katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3470277    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/04/28

Mwanazuoni wa Kisunni Uingereza
Mwanazuoni wa Ki sunni nchini Uingereza amesema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh halitafautishi baina ya Shia na Sunni katika kutekeleza jinai dhidi ya Waislamu.
Habari ID: 3470196    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/03/14

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, wananchi wa Iran wameonesha kivitendo imani yao kwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi uliofanyika nchini hivi karibuni.
Habari ID: 3470191    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/03/11

Sheikhe Mkuu wa Al Azhar, Ahmad Tayyeb ametoa wito wa kufanyika vikao vya pamoja vya wasomi Waislamu wa madhehebu za Shia na Sunni.
Habari ID: 3470188    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/03/09

Bintiye Sheikh Zakzaky
Bi. Nusaiba Zakzaky bintiye Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky ametoa taarifa akibainisha hali ya Waislamu nchini Nigeria na kusema, serikali ya nchi hiyo inawakandamiza Waislamu wa madhehebu zote.
Habari ID: 3468456    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/23

Katika jitihada za kuleta umoja baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, kumefanyika Majlisi za maombolezo Mwezi wa Muharram katika msikiti wa Ma sunni ambapo khatibu alikuwa ni mwanazuoni wa Kishia katika Kituo cha Kiislamu cha Dearborn, Michigan nchini Marekani.
Habari ID: 3391260    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/21

Ayatollah Araki
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kimatiafa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu Ayatollah Mohsen Araki ametoa wito kwa wanazuoni wa Kiislamu kufuatilia suala la kuundwa Umoja wa Nchi za Kiislamu.
Habari ID: 3384011    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/11

Waislamu wa madhehebu ya Shia na wenzao wa Ahlu Sunnah, wamesali pamoja katika moja ya misikiti ya mkoa wa Qatif, mashariki mwa Saudia.
Habari ID: 3324232    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/07

Shekhe Mkuu wa Chuo Kikuu cha kidini cha al Azhar nchini Misri amepinga hatua ya wahubiri wa Kiwahabi na Kisalafi ya kutumia kauli isiyofaa ya ‘Rafidh’ kuwataja Wapenzi wa Ahul Bayt wa Mtume SAW.
Habari ID: 3323156    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/04

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema madola ya kibeberu yanaibua migogoro baina ya Waislamu kwa lengo la kutawala ardhi za Kiislamu zenye umuhimu wa kistratijia.
Habari ID: 2684305    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/07

Mkutano wa 28 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza leo mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu na maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 2684304    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/07

Magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh (ISIL) wameharibu misikiti kadhaa na Haram tukufu za Waislamu wa Sunni na Shia katika mkoa wa Salahuddin nchini Iraq.
Habari ID: 2612443    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/28

Imam Khamenei
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumanne mjini Tehran ameonana na maulamaa, wanavyuoni, wasomi na wageni walioshiriki kwenye Kongamano la Kimataifa la Mirengo ya Kitakfiri kwa Mtazamo wa Maulamaa wa Kiislamu na kulitaja suala la kuzuka upya makundi ya kitakfiri katika miaka ya hivi karibuni kuwa ni tatizo lililopandikizwa na mabeberu katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 2612034    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/26

Wanazuoni waandamizi wa Kishia na Ki sunni nchini Uingereza wamefanya kikao cha pamoja na kujadili njia za kuimarisha umoja miongoni mwa Waislamu sambamba na kukabiliana na kampeni za kuibua fitina katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 1449625    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/09/14

Msomi wa Misri mwenye makao yake Qatar Sheikh Yusuf Qardhawi ametangaza kupinga tangazo la matakfiri wa Daesh la kuanzisha kile wanachokiita eti ni 'Khilafa' au utawala wa Kiislamu katika maeneo waliyoyateka Iraq.
Habari ID: 1426193    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/06