IQNA

Sheikhe Mkuu wa Al Azhar

Maulamaa wa Shia, Sunni watoe Fatwa za kumaliza malumbano ya kimadhehebu

9:31 - July 26, 2016
Habari ID: 3470474
Sheikh Ahmed el-Tayyib, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar, Misri ametoa wito kwa maulmaa wa Shia na Sunni kutoa fatwa ambazo zitawazuia Waislamu wa madhehebu hizo kusitisha malumbano ya kimadhehebu.

Akijibu swali la tovuti ya Kuwait ya al-Anba kuhusu ulazima wa kukurubisha Waislamu wanaofuata madhehebu za Shia na Sunni, Sheikh el Tayyib alisisitiza kuwa hakuna tafauti baina ya Shia na Sunni kwani wote wanaamini kuhusu Tauhidi na Unabii wa Muhammad SAW.

Ameongeza kuwa Al Azhar inafuatilia suala la kukurubisha Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni kama stratijia yake muhimu.

Sheikhe mkuu wa al Azhar pia amewakosoa wale ambao wanalenga kuibua hitilafu na migongano baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni na kubainisha masikitiko yake kuwa watu hawa  hawataki kuzima moto wa  fitina za kimadhehebu.

 

captcha