Akizungumza katika warsha ya "Umoja katika Ummah", jana Jumamosi, Ayatullah Araki alielezea matumaini kuwa wanazuoni na wasomi wa Kiislamu watalipatia uzito suala la kuundwa umoja huo ili kutekeleza matakwa ya Waislamu dunaini ambao wanataka kuona umoja wa kivitendo katika nchi za Kiislamu.
Amesema iwapo nchi tano tu zitaanzisha umoja huo, nchi zingine za Waislamu zitafuata.
Warsha hiyo iliyowaleta pamoja wasomi wa Kishia na Kisuni ilifanyika katika mji wa Lahore nchini Pakistan.
Ayatullah Araki amesisitiza kuwa umoja ni moja ya nukta muhimu zaidi katika ummah wa Waislamu na kuongeza kuwa Waislamu wamehimizwa katika Qur'ani Tukufu na Sunnah ya Mtume SAW kudumisha umoja na kujiepusha na migawanyiko.
Akiashiria kadhia za Syria na Yemen, Ayatullah Araki amewataka Waislamu kutozingatia kinachosemwa katika vyombo vya habari kuhusu migogoro katika nchi hizo. Amesema vyombo vya habari vinajaribu kuonyesha kuwa migogoro hiyo ni ya Sunni-Shia lakini hilo si kweli kwani vita katika nchi hizo ni baina ya mrengo wa muqawama au mapambano kwa upande moja na utawala wa Kizayuni na Marekani kwa upande wa pili.../mh