iqna

IQNA

Harakati za Qur'ani
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa banda la Kurugenzi ya Masuala ya Kidini ya Uturuki (Diyanet) katika Maonyesho ya 34 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran amesema Diyanet inatekeleza shughuli mbalimbali za Qur'ani Tukufu duniani kote.
Habari ID: 3477027    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/21

Hija
TEHRAN (IQNA) - Iran itaanza kupeleka mahujaji wa Hijja nchini Saudi Arabia siku ya Jumatano, Mei 24, afisa mmoja alisema.
Habari ID: 3477022    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/20

Diplomasia
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea ziara yake ya siku mbili nchini Syria kama hatua ya mabadiliko katika kukuza uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama baina ya nchi mbili na kuongeza kuwa lengo kuu la safari hiyo lilikuwa ni kuenzi muqawama au mapambano ya serikali na taifa la Syria.
Habari ID: 3476962    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/05

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ametaja kufeli Marekani katika kuziunganisha nchi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni ushindi au nusra kutoka kwa Mwenyezi Mungu na akaongeza kuwa: "Kumfuata Wali ul Amr wa Waislamu na Hujja za Kisharia ni mfano wa usaidizi wa Mwenyezi Mungu."
Habari ID: 3476960    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/05

Diplomasia
TEHRAN (IQNA) – Rais wa Iran Ebrahim Raisi, ambaye yuko katika safari rasmi nchini Syria, ametembelea kaburi takatifu la Bibi Zainab (SA) huko Damascus.
Habari ID: 3476956    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/04

Diplomasia
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Iran ameashiria kukasirishwa utawala wa Kizayuni kufuatia kuhuishwa uhusiano kati ya Iran na Saudia na akasema: Maadui khususan utawala wa Israel wamekasirishwa na hatua hii na sababu yake ni njama wanazofanya za kueneza migawanyiko.
Habari ID: 3476951    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/03

Diplomasia
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, serikali ya Syria pamoja na wananchi wa nchi hiyo wamepitia masaibu na matatizo mengi na hii leo taifa hilo limeweza kupata ushindi.
Habari ID: 3476950    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/03

Maoni
TEHRAN (IQNA)- Jana, tarehe 10 Ordibehest, 1402 Hijria Shamsia sawa na Aprili 30, ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kufukuzwa wakoloni wa Kireno katika maji ya Kusini mwa Iran hapo mwaka 1622, na inatambuliwa nchini Iran kuwa Siku ya Kitaifa ya Ghuba ya Uajemi.
Habari ID: 3476942    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/01

Mhimili wa Muqawama
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Ijumaa alionana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah na kujadiliana naye masuala muhimu ya pande mbili, ya kieneo na ya kimataifa.
Habari ID: 3476931    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/29

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, jamii ya wafanyakazi wa viwandani haijakubali kutumiwa vibaya na adui na wanaolitakia mabaya taifa la Iran.
Habari ID: 3476930    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/29

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran anasema ukombozi wa Palestina na mwisho wa hali ya janga ambalo Wapalestina wanakabiliwa nalo unakaribia kwani utawala wa Kizayuni wa Israel unaonekana kuwa dhaifu kuliko hapo awali.
Habari ID: 3476928    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/28

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza azma yake katika kadhia ya Palestina na kusema itaendelea kuwaunga mkono wanamapambano wa Palestina katika kukabiliana na vitendo vya kichokozi vya utawala wa Kizayuni.
Habari ID: 3476906    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/24

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Ebrahim Raisi, ameuonya vikali utawala wa kibaguzi wa Israel kuhusu kuchukua hata hatua ndogo ya uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, akisema Iran itajibu uchokozi huo kwa "kuangamiza Haifa na Tel Aviv."
Habari ID: 3476884    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/18

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa iwapo hatua za kimantiki zitachukuliwa, inawezekana kushindwa mahesabu ya adui
Habari ID: 3476877    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/16

Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)- Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamefanyika katika kila pembe ya Iran ya Kiislamu kwa kauli mbiu kuu "Palestina mhimili wa umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu; Quds inakaribia kukombolewa".
Habari ID: 3476864    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/14

Ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Quds
TEHRAN (IQNA)-Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekumbusha wajibu wa kisheria wa mashirika na taasisi za kimataifa na za kutetea haki za binadamu wa kuunga mkono haki za watu walio chini ya utawala ghasibu huko Palestina, na kutoa wito wa kukomeshwa uvamizi huo na kusimamisha jinai za Wazayuni.
Habari ID: 3476862    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/13

Rais wa Iran
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi amesema: taifa adhimu la Iran litatangaza kwa mara nyingine tena kwamba litabaki kuwa thabiti katika malengo ya Uislamu hadi itakapokombolewa Quds kikamilifu, kwa kushiriki kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.
Habari ID: 3476859    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/13

Mashindano ya Qur'ani
TEHRAN (IQNA) – Yunes Shahmoradi kutoka Iran aliyeshika nafasi ya kwanza katika Toleo la 2 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Otr Elkalam nchini Saudi Arabia amesema shindano hilo lilikuwa la kiwango cha juu.
Habari ID: 3476843    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/10

Mashidano ya Qur'ani
TEHRAN (IQNA) - Ifuatayo ni qiraa ya Qari Yunes Shahmoradi kutoka Iran ambaye aliibuka mshindi katika toleo la pili la Shindano la Kimataifa la Qur’ani Tukufu la Otr Elkalam nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3476838    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/09

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amefanya mazungumzo ya simu na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na kutoa wito wa kuitishwa kikao cha dharura cha jumuiya hiyo ili kukabiliana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa.
Habari ID: 3476835    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/08