iqna

IQNA

Mashindano ya Qur'ani
TEHRAN (IQNA) - Iran itashiriki katika mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur'ani nchini Jordan na wawakilishi wawili.
Habari ID: 3476306    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/26

Uislamu na Ukristo
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amewatumia ujumbe wa kheri Wakristo wa Iran na duniani kwa ujumla wakati huu wanapoadhimisha sherehe zao za Krismasi.
Habari ID: 3476304    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/25

Mashindano ya Qur'ani ya Iran
TEHRAN (IQNA)- Finali za Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu Iran zitaanza katika mji mkuu wa Iran, Tehran, mnamo Februari 18, 2023.
Habari ID: 3476285    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/22

Sera za Kigeni za Iran
TEHRAN (IQNA)- Iran imewawekea vikwazo makumi ya maafisa na mashirika ya Umoja wa Ulaya (EU) na Uingereza kutokana na uungaji mkono wao na kuchochea ghasia mbaya za hivi karibuni nchini. Waliowekewa vikwazo wamekuwa wakitoa matamshi yao ya uingiliaji mambo ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu na pia wamekuwa wakiunga mkono uungaji nchini Iran.
Habari ID: 3476240    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/12

Maonyesho ya Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA) - Sekretarieti ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran imesema iko tayari kupokea mawazo na mapendekezo mapya kwa ajili ya kuandaa vyema tukio la kimataifa.
Habari ID: 3476231    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/11

Umoja wa Waislamu
TEHRAN (IQNA)- Kongamano la 18 la kimataifa linalofanyika kwa anuani ya "Uislamu, Uadilifu na Mlingano, Misingi ya Dini na Nidhamu ya Ulimwengu" umeanza rasmi katika mji mkuu wa Russia, Moscow na kufunguliwa kwa salamu za Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3476223    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/09

Rais wa Iran
TEHRAN (IQNA)-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaja Siku ya Mwanachuo kuwa ni nembo ya kumtambua adui, kukabiliana naye, kuwa makini na kuwajibika wanafunzi wa vyuo vikuu.
Habari ID: 3476214    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/07

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi wa Vikosi Vyote vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametilia mkazo kubadilishwa kuwa utamaduni wa watu wote nchini utumiaji uwezo na fursa adhimu za bahari zilizopo.
Habari ID: 3476166    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/29

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) -Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amehutubia hadhara kubwa ya wapiganaji wa kujitolea wa Basiji kwa mnasaba wa Siku ya Basiji ambako amesisitiza kuwa: Mapambano na mapigano makuu ni dhidii ya ubeberu wa kimataifa.
Habari ID: 3476153    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/26

Kombe la Dunia Qatar
TEHRAN (IQNA)- Emir of Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani ameonekana akifurahia ushindi wa Timu ya Taifa ya Soka ya Iran wakati ilipoichapa Wales mabao 2 kwa 0 katika fainali za mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar.
Habari ID: 3476148    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/25

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema lengo kuu la wachochezi wa machafuko ya hivi karibuni ni kuliingiza taifa la Iran katika medani na kuongeza kuwa: "Machafuko hayo bila shaka yatakomeshwa na taifa kuendelea kusonga mbele kwa nguvu zaidi na ari mpya katika uwanja wa maendeleo ya nchi."
Habari ID: 3476116    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/19

Njama dhidi ya Iran
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikwazo vipya vilivyotangazwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya shakhsia 29 na taasisi tatu za Ki iran i, ikiwemo kanali ya televisheni ya Press TV.
Habari ID: 3476094    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/15

Jinai za Marekani
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah amejibu matamshi ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani dhidi ya Lebanon na Hizbullah na kusema: "Marekani ndio msingi wa laana na tauni, na Hizbullah ndiyo iliyoondoa shari na laana ya Marekani nchini Lebanon na kuangamiza tauni hiyo."
Habari ID: 3476074    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/12

Njama dhidi ya Iran
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema njama ya adui ya kuzua ukosefu wa utulivu nchini Iran imefeli sawa na ilivyoshindwa sera ya vikwazo vikali dhidi ya nchi hii.
Habari ID: 3476069    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/11

Jinai dhidi ya Iran
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Intelijensia (Usalama) ya Iran imesema kuwa, vikosi vya usalama nchini vimewatia mbaroni magaidi 26 wakufurishaji ambao walihusika na shambulio la hivi karibuni la kigaidi kwenye Haram Takatifu ya Shah Cheragh katika mkoa wa kusini wa Fars na kuongeza kuwa, mratibu mkuu wa machafuko hayo hatari ni raia wa Jamhuri ya Azerbaijan.
Habari ID: 3476053    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/07

Ustawi wa Iran
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua mfumo mpya wa makombora ya kujihami ya masafa marefu ya Bavar (Kujiamini) 373 na pia imefanyia majaribio kombora jipya la Sayyyad B4 leo Jumapili.
Habari ID: 3476044    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/06

Mwamko dhidi ya Marekani
TEHRAN(IQNA)- Washiriki katika maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu inayosadifiana na leo 4 Novemba, wamesisitiza udharura kuwepo mapambano endelevu dhidi ya njama za kuzusha fitna, ghasia na fujo.
Habari ID: 3476032    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/04

Jibu kwa jinai za Marekani
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa imeyaweka majina ya shakhsia kumi na taasisi nne za Marekani kwenye orodha yake ya vikwazo.
Habari ID: 3476020    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/01

Hujuma ya kigaidi
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Intelijensia (Usalama) ya Iran imetangaza kuwa, imewatambua na kuwatia nguvuni watu sita katika timu ya usaidizi ya magaidi watenda jinai dhidi ya Haram takatifu ya Ahmad bin Musa (AS) maarufu kama Shah Cheragh huko katika mji wa Shiraz.
Habari ID: 3476015    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/10/31

Njama dhidi ya Iran
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa jiji la Tehran na miji yote ya Iran, leo baada ya Sala za Ijumaa, wamefanya maandamano makubwa ya nchi nzima kulaani shambulio la kigaidi lililotokea juzi Jumatano katika Haram Tukufu ya Shah Cheragh ya mjini Shiraz, kusini magharibi mwa Iran. Genge la kigaidi la ISIS limetangaza kuhusika na jinai hiyo.
Habari ID: 3475997    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/10/28