IQNA

Mashindano ya Qur’ani Tukufu

Mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini Uturuki: Qari wa Iran ana matumaini ya Kuingia Fainali

6:31 - June 20, 2024
Habari ID: 3478989
Mwakilishi wa Iran katika kategoria ya kuhifadhi ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Uturuki ana matumaini ya kufuzu kwa fainali.

Qari wa Iran Milad Asheqi, anaiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani nzima huku Sayid Parsa Angoshtan akishindana katika usomaji wa Qur'ani Tukufu  .

Wairani hao wawili walishiriki katika duru ya awali ambayo ilifanyika takriban wiki mbili zilizopita. 

Katika hatua hii, Asheqi alijibu maswali matatu ya jopo la waamuzi kiuhalisia.

Angoshtan, ambaye yuko Makka kama sehemu ya msafara wa Qur’ani wa HIjja wa Iran, alituma faili ya video ya usomaji wake kwenye mashindano hayo.

Asheqi aliiambia IQNA kwamba; alijibu maswali yote matatu kikamilifu na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuwa miongoni mwa washindani wanaofuzu kushiriki katika duru ya mwisho.

Kwa kuzingatia ustadi na kiwango cha juu cha makari na wahifadhi wa Kiirani, kwa kawaida hupita duru za kufuzu kwa urahisi, alibainisha.

Asheqi, ambaye ana tajriba ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Kuwait na Umoja wa Falme za Kiarabu, alisema amepata baadhi ya taarifa kuhusu tukio hilo la kimataifa la Qur'ani la Uturuki.

 Akibainisha kuwa mashindano hayo yatafanyika Oktoba, mwaka huu alisema ana muda wa kutosha wa kufanya mazoezi na kujiandaa kwa hilo.

 Asheqi, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha udaktari, alianza kuhifadhi Quran akiwa na umri wa miaka 8 na kujifunza Kitabu Kitukufu kizima akiwa na miaka kumi.

Alishika nafasi ya tatu katika Mashindano ya 46 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran mwaka jana.

 3488813



captcha