IQNA

Umoja wa Waislamu

Sheikhe Mkuu wa Al-Azhar na Balozi wa Iran wajadili Umoja wa Waislamu

22:07 - September 12, 2023
Habari ID: 3477590
BERLIN (IQNA) - Balozi wa Iran nchini Ujerumani na Sheikhe Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha al-Azhar ncini Misri walikutana mjini Berlin kujadili masuala muhimu yanayoukabili ulimwengu wa Kiislamu na jinsi ya kustawisha umoja na mshikamano kati ya Waislamu.

Mkutano kati ya Mahmoud Farazandeh na Shiekh Ahmad El-Tayyib ulifanyika katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin.
Sheikh El-Tayyib  alionya kwamba hitilafu na migawanyiko iliyopo kati ya Waislamu inatokana na migogoro isiyo ya Kiislamu ambayo Qur'ani Tukufu ilitahadharisha juu yake. Amesema migogoro hiyo inapelekea kupotea kwa umoja wa Kiislamu, kugawanyika kwa jamii ya Kiislamu na kutokuwepo kwa dira ya pamoja baina ya Waislamu.
Ameongeza kuwa licha ya tofauti hizo, Waislamu bado wana malengo ya pamoja ya Kiislamu ambayo wanaweza kuyarejelea. Amesisitiza kuwa, changamoto ya dharura zaidi kwa Ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa ni kuwashawishi wanasiasa na wasimamizi wa maamuzi kwamba maslahi na thamani za Kiislamu ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Alisema kwamba Waislamu wote lazima wakubaliane juu ya kanuni hii.
Aidha amesema wanazuoni wa Kiislamu wamesisitiza mara kwa mara umuhimu wa umoja wa Kiislamu, lakini mara nyingi madola ya kisiasa yanatenda kinyume na mantiki na malengo ya Uislamu.
Alipendekeza kuwa suluhu la mgogoro huu ni kupitisha mfumo wa kimaadili na wa kibinadamu ambao unatanguliza maslahi ya binadamu badala ya ubinafsi.
Balozi Farazandeh alielezea kufurahishwa kwake na kukutana na Sheikh El-Tayyib  na akasifu juhudi zake za kuunganisha ulimwengu wa Kiislamu. Amesema Iran inatambua nafasi ya Kituo cha Kiislamu cha al-Azhar katika kuwaunganisha Waislamu na kuwaongoza kwenye njia sahihi dhidi ya wale wanaojaribu kupotosha sura ya Uislamu.
Pia alisema kuwa Iran imekubali mwaliko wa Sheikh El-Tayyib  wa kushiriki katika mazungumzo ya Kiislamu wakati wa Mazungumzo ya IISS ya Manama mnamo Novemba 2023.

3485140

Habari zinazohusiana
captcha