Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Nickolay Mladenov Mashariki ya Kati amesema kunahitajika muungano wa kimatiafa wa kijeshi ili kuangamiza kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
Habari ID: 3363344 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/16
Maulamaa Waislamu zaidi ya 1,000 nchini India wametoa Fatwa ya pamoja kulaani na kupinga kundi la kigaidi la ISIS au Daesh na kusema harakati za kundi hilo ni dhidi ya mafundisho ya Kiislamu.
Habari ID: 3361079 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/10
Maulamaa Waislamu Ghana
Maulamaa wa Kiislamu nchini Ghana wametangaza msimamo wa kupinga vikali kundi la kigaidi la Daesh au ISIS na kutoa wito kwa vijana nchini humo kuisoma na kufahamu ipasavyo tafsiri ya Qur'ani kwa njia sahihi ili wasitumbukie katika mtego muovu wa ISIS.
Habari ID: 3360612 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/08
Kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) limetekeleza miripuko ya mabomu kwenye msikiti wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia katika mji mkuu wa Yemen Sana'a na kupelekea waumini wasiopungua 32 kupoteza maisha.
Habari ID: 3357626 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/03
Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limeweka sheria kali kwa wakaazi wa mji wa Mosul, Iraq ambao wanataka kuelekea katika safari ya kila mwaka ya ibada ya Hija.
Habari ID: 3354583 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/31
Kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS(Daesh) nchini Iraq, limebomoa msikiti mmoja kusini mwa mkoa wa Nainawa, sanjari na kuondoa nakshi za kihistoria katika makanisa mawili katikati ya mji wa Mosul.
Habari ID: 3353853 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/30
Kundi la magaidi na wakufurishaji wa ISIS (Daesh) kwa mara nyingine wametishia kuibomoa al-Ka'aba katika mji mtakatifu wa Makka.
Habari ID: 3353091 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/27
Wanazuoni wa Kiislamu leo wamemaliza kikao chao Misri ambapo wamejadili ‘fatwa za misimamo mikali’ ambazo zimekuwa zikitolewa na makundi ya kigaidi hasa kundi la kitakfiri la Daesh (ISIS).
Habari ID: 3345846 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/18
Mshtakiwa muhimu zaidi wa shambulio la kigaidi ndani ya msikiti mmoja nchini Kuwait amekiri kuwa ni mwanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.
Habari ID: 3339565 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/06
Kundi la kigaidi na Kitakfiri la Daesh (ISIS) limetangaza kuwapiga marufuku Waislamu kusali Sala ya Idul Fitr baada ya kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3327619 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/13
Baraza Kuu la Maulamaa wa Kiislamu nchini Sudan wametangaza kuwa ni haramu kujiunga na makundi yenye misimamo mikali ikiwemo kundila kigaidi la Daesh au ISIS.
Habari ID: 3325723 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/07
Serikali ya Tunisia imeamua kufunga misikiti 80 inayoendeshwa nje ya udhibiti wake, siku moja baada ya kutokea shambulio la kigaidi na kupelekea makumi ya watu kuuawa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Habari ID: 3320222 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/28
Watu wasiopungua 25wameuawa kufuatia hujuma ya kigaidi iliyolenga msikiti wa Imam Sadiq AS katika mji wa Kuwait.
Habari ID: 3319688 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/26
Magaidi wa kundi la Kitakfiri la Daesh au ISIS wamebomoa makaburi mawili ya kale ya Mawalii wa Allah SWT katika mji wa kihistoria wa Palmyra mkoani Homs nchini Syria.
Habari ID: 3318384 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/24
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kusimama kidete taifa na serikali ya Iraq mbele ya magaidi na Matakfiri ni chanzo cha kudhamini usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.
Habari ID: 3315772 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/17
Khatibu wa Sala ya Ijumaa katika mji wa Najaf, Iraq katika hotuba zake jana amesema kuwa, ‘maeneo mengi ya Iraq yamekomboloewa kutokana na baraka ya fatwa ya Jihad al-Kifai iliyotolewa na Ayatullah Sistani.’
Habari ID: 3313860 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/13
Hata baada ya kupita miezi kadhaa ya kusonga mbele kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika medani za vita kwenye nchi za Kiislamu, Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa serikali ya Washington bado haina stratijia kamili ya kukabiliana na kundi hilo.
Habari ID: 3313196 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/11
Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon
Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon Gebran Bassil amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unafaidika sana na mgogoro baina wa Waislamu wa madhehebu ya Shia na Suni.
Habari ID: 3311306 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/06
Walimwengu wanaendelea kulaani hujuma ya kundi la kigaidi na Kitakfiri la ISIS au Daesh dhidi ya msikiti wa Msikiti wa Imam Hussein AS katika mji wa Dammam mashariki mwa Saudi Arabia.
Habari ID: 3309278 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/05/30
Sheikh Ahmad Khatib, Shekhe Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri ametoa taarifa na kusema kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, ni haramu kubomoa athari na turathi za kihistoria.
Habari ID: 3308489 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/05/27