Katibu Mkuu wa Muungano wa Maulamaa wa Kiislamu Duniani amelitaka kundi la kigaidi la Daesh kuacha mara moja kutenda jinai dhidi ya wanadamu.
Habari ID: 1454356 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/09/27
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei asubuhi ya leo ameruhusiwa kuondoka katika Hospitali ya Shahid Rajai mjini Tehran baada ya kukamilisha matibabu na kupata nafuu kikamilifu.
Habari ID: 1450408 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/09/15
Mufti wa Quds na Ardhi za Palestina Sheikh Muhammad Hussein amesema kuwa kundi la kigaidi la Daesh limefanya matendo yanayopotosha sura ya Uislamu na ni tishio kwa Umma wa Kiarabu na Waislamu.
Habari ID: 1450406 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/09/15
Mufti Mkuu wa Misri, Shawki Ibrahim Abdel Karim Allam amesema kuwa, ni haramu kuunga mkono makundi ya kigaidi.
Habari ID: 1448164 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/09/08
Baraza Kuu la Waislamu nchini Uingereza limelaani ukatili wa kundi la kigaidi la Daesh na kusisitiza kuwa, kundi hilo halina mfungamano wowote na dini Tukufu ya Uislamu.
Habari ID: 1441922 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/23
Mufti Mkuu wa Misri
Mufti Mkuu wa Misri amesema kuwa vitendo vinavyofanywa na kundi la Daesh vinapingana na thamani za kibinadamu na Kiislamu na kwamba kundi hilo ni genge la kigaidi ambalo haliwezi kutambuliwa kuwa ni dola la Kiislamu.
Habari ID: 1439297 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/14
Jumiya ya Nchi za Kiarabu hatimaye imetoa tamko la kulaani jinai zinazofanywa na kundi la kigaidi la Daesh baada ya kimya cha muda mrefu.
Habari ID: 1438344 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/11
Magaidi wa kitakfiri nchini Iraq wameendelea kubomoa turathi za kidini mna maeneno matakatifu ambapo katika tukio la hivi karibuni wamebomoa msikiti wa kale wa Nabii Shayth AS (Seth) katika mji wa Mosul.
Habari ID: 1433798 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/27
Magaidi wa Kiwahabbi wa kundi la kitakfiri la Daesh wamelibomoa na kubakia kifusi kaburi la Nabii Yunus AS lililoko katika mji wa Mosul, nchini Iraq.
Habari ID: 1433174 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/25
Msomi wa Misri mwenye makao yake Qatar Sheikh Yusuf Qardhawi ametangaza kupinga tangazo la matakfiri wa Daesh la kuanzisha kile wanachokiita eti ni 'Khilafa' au utawala wa Kiislamu katika maeneo waliyoyateka Iraq.
Habari ID: 1426193 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/06
Magaidi wa kitakfiri kutoka kundi linalojiita Dola la Kiislamu la Iraq na Sham (Daesh) wamebomoa misikiti na maeneo kadhaa matakatifu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni katika mkoa unaokumbwa na vita wa Nainawa nchini Iraq.
Habari ID: 1426174 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/06
Ayatullah Khatami
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amesema, 'kundi la kigaidi la Daesh ni silaha mpya ya Marekani na madola mengine ya kibeberu inayotumiwa kwa lengo la kuvuruga usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.
Habari ID: 1422882 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/06/27
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa la Waislamu la Iraq litafanikiwa kuwarudisha nyuma magaidi na waungaji mkono wao kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu na kwamba Jamhuri ya Kiislamu itafanya kila iwezalo kulinda maeneo matakatifu nchini Iraq.
Habari ID: 1420250 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/06/19
Ayatullah Ali Sistani, kiongozi mkuu wa kidini wa Waislamu wa Kishia nchini Iraq amewataka raia wa nchi hiyo kujiepusha na aina yoyote ya hatua za kidini au ukabila zinazoweza kuvunja umoja wao sambamba na kuacha matumizi ya silaha kinyume cha sheria.
Habari ID: 1418402 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/06/16
Harakati za kundi la kigaidi la DAESH katika maeneo mbalimbali ya Iraq zimekuwa sababu ya mshikamano na umoja kati ya makundi mbalimbali ya taifa la nchi hiyo.
Habari ID: 1417080 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/06/13