IQNA

Fatwa ya Ayatullah Sistani imeiokoa Iraq

18:38 - June 13, 2015
Habari ID: 3313860
Khatibu wa Sala ya Ijumaa katika mji wa Najaf, Iraq katika hotuba zake jana amesema kuwa, ‘maeneo mengi ya Iraq yamekomboloewa kutokana na baraka ya fatwa ya Jihad al-Kifai iliyotolewa na Ayatullah Sistani.’

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sayyid Saddrdin al Qubanchi, Imam wa Sala ya Ijumaa mjini Najaf al Ashraf akiashiria mwaka moja tangu itolewe fatwa ya 'Jihad al-Kifai' na Ayatullah Ali al-Sistani amesema: “Kujitolea wananchi kufuatia fatwa hiyo kumepelekea kupatikana mafanikio makubwa zaidi katika historia ya kisasa ya Iraq. Wananchi wamejitolea pasina kutarajia malipo wala faida zozote za kidunia.”

Akiashiria uamuzi wa Marekani kutuma askari 500 nchini Iraq amesisitiza kuwa, “Iraq haihitajii vikosi vya kigeni bali kile ambacho kinaisumbua ni ukosefu wa silaha za kutosha vitani.”
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi naye pia amegusia fatwa ya Ayatullah Sistani kuhusu ulazima wa kupambana na magaidi wa kitakfiri wa ISIL au Daesh na kusema, fatwa hiyo imeiokoa Iraq kutokana na njama kubwa ya maadui.


Mwaka moja uliopita, Ayatullah Sistani, kiongozi wa ngazi za juu zaidi wa Kishia nchini Iraq alitoa fatwa akisema ni wajibu wa kidini kusimama na kupambana na magaidi wa Kitakfiri na kuwatimu Iraq. Alitoa wito kwa Wairaqi wote kujitolea muhanga kuilinda nchi yao na matukufu ya kidini.../mh

3313465

captcha