Sikukuu ya Idul Fitr
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei anasema utawala wa Kizayuni wa Israel "lazima uadhibiwe na kutiwa adabu" kwa shambulio lake baya dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
Habari ID: 3478662 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/10
Salamu za Idul Fitr
IQNA-Rais wa Iran, Ebrahim Raisi, amesema ni wajibu wa kibinadamu na kidini kwa nchi za Kiislamu kukomesha mauaji ya kimbari ya miezi kadhaa ya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
Habari ID: 3478661 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/10
Mrengo wa Muqawam
IQNA- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amesema, haki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kutoa jibu kwa uchokozi uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa kushambulia ubalozi wake mdogo mjini Damascus ni haki yenye uhalali wa kisheria.
Habari ID: 3478656 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/09
Siku ya Quds
IQNA-Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) anasema utawala wa Kizayuni wa Israel utasambaratika hivi karibuni, akibainisha kuwa Marekani inaiunga mkono waziwazi Israel.
Habari ID: 3478634 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/05
Siku ya Quds
IQNA-Mamillioni ya wananchi wa Iran wamejitokeza katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo yamefanyika leo katika miji na maeneo mbalimbali nchini Iran.
Habari ID: 3478633 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/05
Kadhia ya Palestina
IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu ni tofauti na miaka iliyopita, na kwamba operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imemweka adui Mzayuni kwenye ukingo wa shimo la mauti.
Habari ID: 3478629 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/04
Jinai za Israel
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Majenerali walioongoka wa Kiislamu katika shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria na kusisitiza kwamba: "Taifa la Iran litawafanya Wazayuni wajutie jinai hiyo na jinai zingine kama hiyo."
Habari ID: 3478616 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/02
Diplomasia ya Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, Muqawama (mapambano ya Kiislamu) usio na kifani wa vikosi vya Muqawama na watu wa Ghaza umeutukuza Uislamu.
Habari ID: 3478588 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/27
Ukanda wa Gaza
IQNA – Mjumuiko mkubwa wa futari umefanyika katika mji wa Rafah, kusini mwa Gaza, licha ya kuendelea mashambulizi ya utawala haramu Israel dhidi ya mji huo.
Habari ID: 3478586 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/26
Kadhia ya Palestina
IQNA-Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Afrika Kusini amesema kuwa, raia yeyote wa nchi hiyo atakayeusaidia utawala wa Kizayuni katika vita vya Ukanda wa Gaza atatiwa mbaroni punde tu atakaporejea Afrika Kusini.
Habari ID: 3478520 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/16
Wapalestina katika Mwezi wa Ramadhani
IQNA - Rais wa Jumuiya ya Wahubiri wa Kiislamu Palestina ametoa wito kwa Waislamu wote wanaofunga mwezi mtukufu wa Ramadhani waombe dua kwa ajili kukomeshwa mateso na masaibu wanayokumbana nao watu wa Gaza.
Habari ID: 3478495 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/12
Ramadhani Palestina
IQNA - Waislamu wa Palestina huko Gaza wamebakia imara katika Imani na hivyo wana azma ya kutekeleza ibada zote za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kukusanyika katika mabaki ya misikiti iliyoharibiwa na mabomu ya utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3478485 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/10
Watetezi wa Palestina
IQNA-Maandamano makubwa yamefanyika mbele ya ubalozi wa Israel mjini Washington DC, Marekani kulaani vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478443 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/03
Jinai za Israel
IQNA - Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kusikitishwa kwake na ukatili ambao utawala wa Israel imekuwa ukitekelezwa kwa miezi kadhaa vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478435 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/01
Jinai za Isarel
IQNA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesikitishwa na mauaji ya utawala haramu wa Israel dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza, akisema hali hiyo inatishia sheria za kimataifa za kibinadamu.
Habari ID: 3478420 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/27
Jinai za Israel
IQNA - Kutakuwa na mlipuko na maafa makubwa hivi karibuni ikiwa utawala wa Kizayuni utaendelea na mpango wa kuwazuia Waislamu kuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ilionya.
Habari ID: 3478412 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/25
Jinai za Israel
IQNA-Mkuu wa Kitengo cha Asia Magharibi katika Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema: Idadi ya raia na waandishi wa habari waliouawa huko Gaza haina mfano.
Habari ID: 3478363 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/16
Watetezi wa Palestina
IQNA - Hatua za kivita za utawala wa Israel huko Rafah "zinathibitisha" usahihi wa kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya utawala huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema.
Habari ID: 3478356 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/15
Watetezi wa Palestina
IQNA-Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimelaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza, na kuonya kuhusu maafa ya binadamu katika eneo hilo.
Habari ID: 3478350 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/14
Jinai za Israel
IQNA-Utawala katili wa Israel umeendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kwa kutekeleza mashambulizi makubwa ya anga na mizinga katika mji wa Rafah kusini mwa ukanda huo na kuua na kujeruhi mamia ya raia wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Habari ID: 3478339 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/12