israel - Ukurasa 10

IQNA

Jinai za Israel
IQNA - Jumla ya misikiti 604 imeharibiwa kabisa katika Ukanda wa Gaza hadi sasa kutokana na mashambulizi ya utawala wa Israel katika maeneo ya makazi na yasiyo ya kijeshi.
Habari ID: 3478843    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/18

Watetezi wa Palestina
IQNA - Wakati wa warsha iliyofanyika katika maonyesho ya sanaa yanayoendelea Tehran idadi kubwa ya waandishi wa kaligrafia wameandika Surah Al-Fil ya Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 3478841    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/18

Jinai za Israel
IQNA-Afrika Kusini imeitaka Mahakama Kuu ya Umoja wa Mataifa iamuru kusitishwa uvamizi wa kijeshi dhidi ya Rafah kama sehemu ya kesi yake iliyofungua mjini The Hague inayoushutumu utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mauaji ya kimbari, ikisema utawala huo "lazima uzuiwe" ili kunusuru maisha ya Wapalestina.
Habari ID: 3478840    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/17

Ukombozi wa Palestina
IQNA-Ismail Haniyah, Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema bila shaka utawala wa Kizayuni wa Israel hatimaye utaondolewa katika maeneo yote ya Wapalestina.
Habari ID: 3478831    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/16

Watetezi wa Palestina
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimekaribisha uungwaji mkono wa nchi hiyo kwa hatua za kisheria zilizochukuliwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala haramu Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
Habari ID: 3478819    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/14

Jinai za Israel
IQNA-Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetoa mwito wa kukomeshwa mauaji ya kiholela dhidi ya Wapalestina, hasa watoto wadogo katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478818    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/14

Jinai za Israel
IQNA - Balozi wa Afrika Kusini nchini Iran amesema zile siku za utawala wa Israel kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina bila kuadhibiwa zimefika ukingoni.
Habari ID: 3478802    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/10

Jinai za Israel
IQNA-Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, Ismail Haniyah amemfahamisha kuhusu jibu la Hamas kwa pendekezo la kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478785    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/07

Watetezi wa Palestina
IQNA - Vuguvugu la wanafunzi wanaounga mkono Palestina, wanaokabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel, limeenea kote nchini Marekani licha ya ukandamizaji wa polisi, huku wanafunzi wa vyuo vikuu vingi kama vile Yale, New York, Harvard, Texas huko Austin, na Kusini mwa California wakijiunga nayo.
Habari ID: 3478759    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/03

Mauaji ya Kimbari Gaza
IQNA - Ili kushughulikia mahitaji ya dharura zaidi ya Wapalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limewasilisha ombi la dharura la msaada wa  dola bilioni 1.21.
Habari ID: 3478731    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/25

Kadhia ya Gaza
IQNA-Maandalizi yanaendelea na Muungano wa Kimataifa wa Msafara wa Meli wa Uhuru, unaoundwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka nchi kadhaa, ili kupeleka misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza unaokabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3478704    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/20

Ahadi ya Kweli
IQNA - Mchambuzi wa Lebanon ameorodhesha nukta nane kuhusu mashambulizi ya kulipiza kisasi wa Iran dhidi ya utawala haramu wa Israel ambayo yalikuja baada ya mashambulizi ya Israel kwenye ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria.
Habari ID: 3478691    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/16

Ahadi ya Kweli
IQNA - Msururu wa vikao vha kusoma  Qur'ani Tukufu ambavyo vimepewa jina la "Ahadi ya Kweli" vinafanyika katika Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.
Habari ID: 3478689    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/16

Jinai za Israel
IQNA - Barabara kuu ya 101 ya San Francisco kwenye daraja la Golden Gate ilifungwa na waandamanaji wanaounga mkono Palestina wakitaka kukomesha uungaji mkono wa Marekani kwa utawala katili wa Israel ambao unaendeleza vita vya mauaji ya kimbari Gaza.
Habari ID: 3478688    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/16

Ahadi ya Kweli
IQNA-Mufti Mkuu wa wa Oman amekaribisha na kupongeza mashambulizi ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3478687    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/16

Ahadi ya Kweli
IQNA-Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameionya Marekani kuhusu kuanzisha hatua za kijeshi dhidi ya Iran baada ya operesheni yake ya kisheria ya hivi karibuni ya kulipiza kisasi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, mshirika mkuu wa kieneo wa Washington.
Habari ID: 3478686    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/15

­­­­­­­­­Ahadi ya Kweli
IQNA-Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utafanya harakati yoyote ya kifidhuli utakabiliwa na jibu madhubuti, zito na kali zaidi.
Habari ID: 3478685    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/14

Ahadi ya Kweli
IQNA- Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limefanya mashambulizi makubwa ya kulipiza kisasi kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel likijibu mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa utawala wa Israel ya tarehe 1 Aprili dhidi ya majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
Habari ID: 3478681    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/14

Kadhia ya Palestina
IQNA-Viongozi wa Ireland na Uhispania wametangaza kuwa nchi kadhaa za bara la Ulaya zinakaribia kutambua rasmi nchi huru ya Palestina.
Habari ID: 3478676    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/13

Jinai za Israel
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani mauaji yaliyofanywa na jeshi la utawala katili wa Israel dhidi ya wanafamilia wa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478673    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/12