IQNA

Jinai za Israel

Daraja la Golden Gate la San Francisco lafungwa kuuunga mkono Gaza (+Video)

16:51 - April 16, 2024
Habari ID: 3478688
IQNA - Barabara kuu ya 101 ya San Francisco kwenye daraja la Golden Gate ilifungwa na waandamanaji wanaounga mkono Palestina wakitaka kukomesha uungaji mkono wa Marekani kwa utawala katili wa Israel ambao unaendeleza vita vya mauaji ya kimbari Gaza.

Waandamanaji hao walizuia magari kwenye daraja hilo siku ya Jumatatu.

Huku wakisimamisha magari yao na kuziba njia zote za kuelekea kusini, waandamanaji hao waliitaka Marekani kuacha kuupa silaha na kuufadhili utawala wa Israel katika vita vinavyoendelea Gaza.

Waandamanaji walibeba mabango yenye maandishi “Simamisha Ulimwengu kwa ajili ya Gaza” na “Komesha Kuzingirwa kwa Gaza Sasa.”

Israel ilianzisha vita dhidi ya Gaza Oktoba 7 baada ya operesheni ya kulipiza kisasi ya wapigani ukombozi wa Palestina na hadi sasa jeshi katilila Israel limeua takriban Wapalestina 33,800, wengi wao wakiwa wanawake na watoto na wengine 76,500 kujeruhiwa huku kukiwa na uharibifu mkubwa na uhaba wa mahitaji.

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki katika kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini ambapo mwezi Januari mahakama hiyo ilitoa uamuzi wa muda ikiiamuru Israel kuhakikisha vikosi vyake havifanyi mauaji ya kimbari. Hatahivyo kutokana na uungaji mkono wa Marekani, Israel imekaidi amri ya mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa.

3487958

Habari zinazohusiana
captcha