IQNA

Jinai za Israel

Balozi wa Afrika Kusini: Zama za Israel kutekeleza mauaji ya kimbari bila kuwajibishwa zimekwisha

20:46 - May 10, 2024
Habari ID: 3478802
IQNA - Balozi wa Afrika Kusini nchini Iran amesema zile siku za utawala wa Israel kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina bila kuadhibiwa zimefika ukingoni.

Francis Moloi aliyasema hayo katika kikao maalumu kilichofanyika mjini Tehran chini ya anuani ya "Afrika Kusini na Mjadala wa Muqawama", Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) limeripoti.

Ameashiria hatua ya Afrika Kusini ya kuwasilisha malalamiko dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) na kusema ni kutokana na utawala wa Israel kukiuka majukumu yake ya kimataifa kwa mujibu wa Mkataba wa Kuzuia Mauaji ya Kimbari.

Ameashiria pia malalamiko kutoka nchi nyingine kama Bolivia, Bangladesh, Visiwa vya Comoro na Djibouti katika ICJ kuhusu jinai za mauaji ya kimbari zinazoendelea kutekelezwa na Israel katika Ukanda wa Gaza.

Moloi alitabiri kwamba katika siku za usoni, hukumu zitatolewa dhidi ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Israel.

Mwanadiplomasia huyo wa Afrika Kusini pia alisema kuwa wananchi katika mataifa mbali mbali ya dunia wanashinikiza serikali zao kuunga mkono haki za Wapalestina.

Aliendelea kusema kuwa katika wakati ambapo Israel inapata uungwaji mkono wa kijeshi kutoka kwa nchi za  Magharibi, "Tunategemea nguvu za kiraia waliowengi katika nchi hizo na tunahisi kuimarika nguvu za kuunga mkono Palestina."

Israel ilianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7.

Zaidi ya Wapalestina 34,800 wameuawa tangu wakati huo huko Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine 78,400 wamjeruhiwa.

Kutokana na mashambulizi ya zaidi ya miezi saba ya Israel, maeneo mengi ya  Gaza sasa ni magofu, na kusukuma 85% ya wakazi wa eneo hilo kuwa wakimbizi wa ndani huku kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa, kulingana na UN.

Israel inalaumiwa kutekeleza mauaji ya kimbari katika mahakama ya ICJ. Uamuzi wa muda wa mwezi Januari wa ICH ulisema "inawezekana" kwamba Israel inahusika na mauaji ya kimbari Gaza na hivyo mahakama hiyo iliiamuri Israel isitishe vitendo  hivyo hata hivyo utawala wa Kizayuni umekaidi amri ya mahakama hiyo.

Days of Israeli Genocide with Impunity Over: South African Envoy

 

Days of Israeli Genocide with Impunity Over: South African Envoy

 4214704

Habari zinazohusiana
captcha