IQNA

Watetezi wa Palestina

Waandishi 100 wa Kaligrafia Iran waandika Surah Al-Fil katika mfungamano na mshikamano na Wapalestina

21:15 - May 18, 2024
Habari ID: 3478841
IQNA - Wakati wa warsha iliyofanyika katika maonyesho ya sanaa yanayoendelea Tehran idadi kubwa ya waandishi wa kaligrafia wameandika Surah Al-Fil ya Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa taarifa, waandishi 100 wa kaligrafia kutoka mikoa 10 ya Iran walishiriki katika mpango huo.

Hafla hiyo ya ilihusu risala ya sura ya 105 ya Qur’ani Tukufu, ambayo inahusu kuangamizwa kwa jeshi la maadui wa Mwenyezi Mungu kupitia  makundi ya ndege. Wanakaligrafia hao walijumuika kufungamana na Wapalestina ambao wanakabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala katili wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Maandishi hayo ya kaligrafia ya Sura Al Fil yameandikwa  kwenye maonyesho, ya Qur’ani Tukufu yaliyopewa jina la "Simulizi ya Mvua", ambayo yanaendelea katika Kituo cha Utamaduni cha Niavaran huko Tehran.

Maonyesho hayo ya sanaa ya Qur'ani yameratibiwa na Jumba Maalum la Sanaa za Iran na Kiislamu na yataendelea hadi Mei 20.

Utawala ghasibu wa Israel ulianzisha mashambulizi ya kikatili kwenye Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7, 2023 na kuendeleza vita vya mauaji ya halaiki licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano katika eneo hilo.

Zaidi ya Wapalestina 35,200 wameuawa tangu wakati huo, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine zaidi ya 79,200 wamejeruhiwa tangu Oktoba mwaka jana kufuatia shambulio la kundi la Hamas la Palestina.

Zaidi ya miezi saba ya vita vya Israel, maeneo makubwa ya Gaza yalikuwa magofu huku utawala huo wa Kizayuni unaopata himaya ya Marekani ukuzuia misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo..

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo imeiamuru Tel Aviv kuhakikisha kuwa vikosi vyake havifanyi mauaji ya halaiki na kuchukua hatua za kuhakikisha misaada ya kibinadamu inatolewa kwa raia huko Gaza. Hatahivyo utawala dhalimu wa Israel umepuuza agizo hilo la Mahakama ya Kimataifa ya Haki.

3488369

Habari zinazohusiana
captcha